22.11.13

Saturday, March 20, 2010

TURUDI SHULE KIDOGO...

Hii ni shule ambayo ipo maeneo ya Bagamoyo si mbali sana na Bagamoyo Town inajulikana kwa jina la NIANJEMA HIGH SCHOOL, shule hii bado mpya sana na ina kidato cha kwanza hadi cha tano. Ina walimu wazuri wanaojua kufundisha masomo na mpaka mwanafunzi akafaulu mitihani ya National.

Hapa ni sehemu ya kukutana wanafunzi na walimu majira ya asubuhi na baadaae huruhusiwa kwenda madarasani.

Madarasa kama yanavyoonekana yakiwa yamejipanga na mengine yapo kwa nyuma yakijengwa

Mwanafunzi anapokuwa eneo la shule basi kiswahili kinatupwa kulee halafu mpango mzima unakuwa ni ngeli kwa kwenda mbele i mean SPEAK ENGLISH ONLY.

Miti yakutosha na hali ya hewa ni safiiiiiiiiiiii wala hakuna utata kabisa, swala la msingi ni mzazi au mlezi kama unaangaika kutafuta sehemu yakumsomesha mtoto au mdogo wako basi fika shule hii iliyopo Bagamoyo ili apate elimu bora kabisa.

2 comments:

Anonymous said...

Shule ni nzuri sana jamani....natamani ningekuwa mwanafunzi tena

Anonymous said...

choka bora kidogo uwe unapitia pitia na shule ili kuona shule zetu zikoje..sisi wahuku mbali tunahamu kweli kweli...big up choka