22.11.13

Sunday, September 12, 2010

EID PILI ILIVYOJAZA WATU NDANI YA COCO BEACH KWENYE UZINDUZI WA tiGO PESA.

Wakati tupo kwenye gari mimi pamoja na Joh Makini, Gnako na Bonta tulikuwa hatumamini tunachokiona pale Coco Beach jinsi watu walivyofurika na foleni ya magari hadi ikabidi kupaki gari barabarani na kuanza kutembea kwa miguu ili kuwahi stejini.

Kule mwisho ni Gnako, Bonta katikati na Dj Choka

Hatimae tuliwahi show na watu wazima wakawa stejini na me nikawa huku nyuma ya watu ni ki dj show huku nikipiga picha..daaah kuna saa natamani mwili wangu ujigae mara mbili natamani ningekuwa na uwezo wakuwa na wasaidizi wengi sehemu kama hizi hazinipi shida

Bahada ya show watu sasa wanaanza kutafuta usafiri wakurudi lakini nimejifunza kitu kimoja, hivi kwanini nyie mnaoenda na watoto wadogo sehemu kama hii mnakuwa mnastarehe hadi kuwasahau watoto wenu jamani....
Kuna watoto kama 6 hivi walikuwa wamesimama mbele yangu wakilia mama mamaa daah iliniuma sana nasikitika sikuweza kuwapiga picha kwasababu zilizo nje ya uwezo wangu.

2 comments:

staboka said...

Djchoka nakukubali maana mambo yako si mchezo! Picha zote zimekwenda darasa! Nimefurahi sana kwa Blog yako! Big up Man and Keep it on!

staboka said...

Mkubwa nakukubali! mambo yako mpango mzima ni byee!