22.11.13

Tuesday, December 04, 2012

Baada ya PAMOJA WE CAN sasa ni PRESS PLAY "DJ CHOKA"

Najua nilikaa mda mrefu baada ya kutoa wimbo wa PAMOJA WE CAN, sasa nimeona mwaka usiishe hivi hivi ngoja niwape madini mengine baada ya kusign na B'Hitz Music Group. Sasa ni zamu ya PRESS PLAY ambayo ni DJ Choka feat. M-Rap, Gosby, Mabeste & Deddy, kwa upande wangu wimbo ni mzuri na kwenye Production kasimamia Pancho Latino na Mixing kasimamia kaka mkubwa Hermy B. 

Baada ya kuutoa wimbo huu nitatoa video yake, nilikuwa nataka kutoka kwa mpigo ila uwongozi wa Bhitz ukaniambia tuanze na Audio halafu video inafuata so lazima nifuate protoko. Natumaini mtaupokea vizuri kwa sababu nia na madhumuni sio mimi nitoke hapana nia na madhumuni ni kutoa wasanii wapya lakini kwa sasa naadha na wasanii wangu ambao tuko wote Bhits halafu watafuata wasanii wachanga wengine mwakani. 

1 comment:

thegreat mpagati said...

Mzigo umesimama vilivyo, big up 2 djchoka!!!