Jina la mtoto anaitwa Ombeni
Mbeula
Mama wa mtosto anaitwa Kilaudia
Kigaila
Nyumba iliungua wakati watoto hao
wamekaa ndani na wakati huo huo mama wa mtoto alikuwa amekwenda shambani maeneo
ya Chitemo iliyoko wilaya ya mpwapwa
Wakati mvua inanyesha ghafla nyumba
ilibomoka na wakati huohuo walikuwa watoto wawili walikuwa jikoni ndani ya hiyo
nyumba. Baada ya tukio hilo kutokea ikafanyika uokoaji kwenye
nyumba hiyo maeneo ya Chitemo na kufanikisha kuokoa watoto
wote wawili kati ya mmoja aliumia kwa kuangukiwa na udongo wa nyumba hiyo na
huyu Ombeni Mbeula aliangukia kwenye moto mpaka kuungua hivi unavyoona kwenye
picha lakin hali zao ni salama kwa wote.
Baada ya uokoaji waliamua kumpeleka
mtoto huyo kwenye hospitali ya Mima iliyoko Mpwapwa ikashindikana madaktari
wakamuagiza aende hospitali ya Mpwapwa hapo hospitalini wakakaa siku mbili
katika hospitali ya mpwapwa na siku ya tatu wakaambiwa waende
hospitali ya rufaa iliyoko Dodoma Mjini ambayo ni inajulikana General kwa matibabu
zaidi.
Walipofika katika hospitali ya mkoa
wa Dodoma wakaanza matibabu lakini uwezo wa kipato cha wazazi wake sio kizuri
inahitajika msaada kwa matibabu maana hata dawa hajapatiwa na pesa kwa ajili ya
matibabu haikuweza kupatikana paka sasa
Kama umeguswa kutoa ni moyo sio
utajiri muokoe mtoto huyu maana hata kula anashindwa mpaka kuona anaona kwa
mbali sana.
Mama yake hana simu lakini anatumia
simu ya ndugu yake Ekiria Paskali
Kwa yeyote atakayependa kumchangia
mtoto huyo atume chochote kwenye namba hii au atumie M- pesa kwenye namba hii
0757 498336
PICHA KWA HISANI YA PAMOJAPURE BLOG
No comments:
Post a Comment