Monday, February 11, 2013

Weekend yangu iliyopita nilikuwa MIKUMI NATIONAL PARK

Weekend yangu iliyopita nilikuwa Mikumi National Park kwenye utalii wa ndani na nilipata mwaliko huo kupitia kampuni ya Lakeland Africa ambao hufanya kazi za kuwasafirisha watalii nchini na nje ya nchi. Sio mimi tu niliyealikwa walikuwepo wasanii wawili wa bongo fleva Mabeste na Cyrill pamoja na Miss East Africa anayetokea Tanzania anajulikana kwa jina la Jocelyn Maro. 

Kama unataka kufanya tour ya kwenda mbugani au sehemu yoyote kuangalia history ya nchi yetu basi mnakaribishwa na unaweza kuwasiliana na LakeLand Africa kwa namba hizo hapo chini

Lakeland Africa is Tanzania's leading provider of group overland budget travels and car rental services to corporate Tanzania and business travellers:
+255 222 76 18 11, + 255 784 88 59 01 
Email: reservations@lakelandafrica.com
Hapa tukiwa kwenye bwawa wanaloishi viboko na nilikuwa najaribu kumuonyesha Miss East Africa kwamba hawa wadudu wakitoka nje ya maji sisi tunaonekana kama sisimizi hahaaa

Toka nizaliwe kiukweli sijawahi kulala porini kwenye haya mahema, na kiukweli nilikuwa naogopa sana usiku maana daaah yataka moyo lakini ilipofika asubuhi niliona kitu cha kawaida sana na nikasema kweli unaenjoy hewa safi sana na usingizi unakuja vizuri kabisa 

 Baada ya kuzunguka mchana kutwa kuchek wanyama usiku ikawa ni bata mdogo mdogo nikiwa na ndugu yangu Mabeste #TeamBhitz

No comments:

Post a Comment