22.11.13

Thursday, April 04, 2013

(News) KITALE AWAOMBA RADHI WAISLAM WOTE.

Mchekeshaji maarufu hapa kwetu Bongo anayejulikana kwa jina la KITALE hivi leo kuna mtu amegundua password ya account yake ya facebook na huyo mtu kuingia kwenye Wall ya Kitale na kuandika matusi kuikashifu dini ya kiislam. Kitale ameongea na DJCHOKAblog na kuwaomba radhi kwa kitendo kilichotokea na samahani kwa yoyote aliyekwazika kwa kitendo hicho. 

Haya ni maneno aliyoyaandika KITALE baada huyo mtu kuandika matusi katika ukurasa wake wa Facebook NANUKUU.

"Assalam Aleykum kwa wale WAISLAM NA WASIOKUA WAISLAM, SAMAHAN SANA NDUGU ZANGU KUNA MTU AMEFANYA HIKI KITU PASIPO MWENYEWE KUJUA NA BAADA YA KUPIGIWA SIMU NA MASHABIKI WANGU KUA KUNA KITU KAMA HIKI NIMEJISIKIA VIBAYA SANA KUTOKANA NA MIMI MWENYEWE NI MUISLAM SAFI NA SIO TEJAH KAMA NINAVYOIGIZA. HIVYO NAOMBA RADHII NDUGU ZANGU..!! HATA PIA HUYU MTU ALIKUA ANAWATUMIA WATU MESSAGE KWENYE INBOX KUWAAMBIA KWAMBA NIPO DAR, NAWATHIBTISHIA KWAMBA MIMI NI KITALE NA SASA NIPO KAHAMA...!!!"

No comments: