22.11.13

Wednesday, May 01, 2013

(News) Alichokiandika LADY JAYDEE kupitia BLOG yake "WOSIA WANGU KAMA IKITOKEA NIMETANGULIA KUFA KABLA YA RUGE AU JOE KUSAGA"

Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi
Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.

Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.

Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.

Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa.
Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive bila wao.

Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria.
Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.

Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia.
Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa.

Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao.
Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.

Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu.

Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige wame
Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.

Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai
Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu.
Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.

Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge.
Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.

Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia..
Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..

Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.
Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.

Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili.
Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.
Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani??
Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??

Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili.

Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu.
Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma??
Roho gani hiyo??

Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu

JIDE

22 comments:

mkuuuuuuubwa said...

vinega na antivirus walionekana wakorofi. na huyu dada yetu je. this bongo music will never expand till viruses are killed. jaydee find the other ways to save other underground artists. who are downpressed. InI Jah Rastafarai

Anonymous said...

Wanafiki hao achana nao!

mentire said...

Wafu fm ndo wanaua game ya bongo kwa kupromote wasanii wasio na uwezo na kuwabania wenye uwezo wao mamaeee zao!

Anonymous said...

Duuuhhh... Pole saana my dada.... Inauma lakini poa.. Pigana kikike amini utaishinda vta hii...

Unknown said...

Pole nasoma haya kwa uchungu mkubwa ila mungu ni muweza umesema naamini umeongeza umri wako na ubaki mwepesi kiroho wanamtandao mkubwa sana na pia ma manage wana fitna hizo hakuna msanii aliyewatajirisha kama kibra nature wamenyonya mpaka dam wapo wengi wanaotaabika kama wewe hila kwakua hawawezi kusimama peke yao wanavumilia huku wakiumia rohoni.... Ombea adui yako aishi siku nyingi ili unavyobarikiwa wajionee kwa macho.

Anonymous said...

Kwa nini usijiunge na SUGU muendeleze mapambano? Vile vile kumbuka kujiunga na watu wa GWANDA sababu hawa wawili unaowasema ni sehemu ya tatizo kubwa sana. Sugu alishayaona haya ndo maana ana GWANDA lake siku nyingi tu! Pole sana kamanda Anaconda.

Anonymous said...

Dah,gud cster and <3 u a sms hvi ndivyo inavyotakiwa uwe na msimamo na unachokisema @segret don skillz

Anonymous said...

Jide lv u ma sis. Dnt wry dia Hakuna atakayezba milango ya baraka God aliyokufungulia hop one day God ataanika uovu wa wanafiki I hop dat.Mrs.S

james mbegeze said...

dah no comments

Anonymous said...

game la bongo halina usalama hata kidogo na Media zingine zimekubali utawala wa Clouds!!! hazitafuti njia mbadala ya kujiimarisha katika burudani na mziki kwa ujumla..... Jide unawashabiki lukuki Dunian kwa ujumla na ni M/ke unayejitambua sana so FANYA YAKO hakuna awezaye bila MUNGU

Anonymous said...

wachane vilaza hao, wanaokula kwa jasho la wenzao!

Anonymous said...

Umetisha xan jide ila utaona wanafiki wanaotaka kuuwa game watakavyo kurushia maneno. La mcng,big up kaz but komand.

Wizzle said...

Jd Umeonesha msimamo kama wanaume yaaani Vinega dawayao ho Wafu nikuzidishakiburi dhidi yaoo nakuwaelimisha wasanii wengineoo Hongera saaaana dada kwa msimamo uloutoa

Wizzle said...

Game la Bongo fitna xaaaaaaana yan Big up kwakutuweka waz mwanadada

Anonymous said...

BIG Up sis jideeeee,naamini ww ni komando kiukweli.hawa clouds washenzi tu wanaona wao ndo wao bongo.lakin naimani kukuchukia ww basi watapoomoka wao

Anonymous said...

aisee wr kweli komando.amini mungu ndo muweza kama wana uwezo wa kuinua vipaji wainue vya madem zao.ipo cku watanzania wote wataujua ubaya wao.

Anonymous said...

Vinega movement ya Antvirus vip? Tunasubiri volume 3. Nakumbumbuka ile mistari yenu kwamba tuna dada zetu kaka zetu wanatuangalia tunafanya nin acheni mambo yenu mamaee zenu.

Anonymous said...

Pole mamii jitahidi kusamehe hii dunia tunapita tuu

Anonymous said...

hao wa haya hawana maana achana nao pia wamejaribu kumuua p.funk majani ambaye aliyesababisha umaarufu wa cloudz fm ukoloni tulidhani umeisha kumbe bado upo mpaka le9?

Anonymous said...

clouz sio ppz station wametuulia sanaaa wasanii wtu wengiii jaman tz tubadilike tutazame maslai ya wanamuzki wetu wanaojituma kam jide na wengine wengiii

Anonymous said...

jide ni bora kuliko clouz

Anonymous said...

Wachane wanajidai miungu watu sana hawa.....wanawapeleka peleka wasanii kama wake zao,huku wakijidai wao ndo wanaukuza muziki wa kibofongo kumbe ndio wadidimizaji wakubwa.....ila ikosiku watajua kwamba jasho la mtu haliendi kirahic.