22.11.13

Thursday, July 25, 2013

(Audio & Lyrics) Stamina ft. Darasa & Warda - Mwambie Mwenzio

Song:Mwambie Mwenzio
Artists:Stamina ft Darasa&Warda
Studio:One Love Fx
Producer:Tiddy Hotter
Song writers;sStamina(verses)Darasa(choruss)
Intro:(stamina)
stamina)……you what tiddy?this is one love fx,shorwebwenzi on this one,itc moro town beiiib

vers 1(stamina)
wakuja rudi bushi,mji unahitaji waliosoma.
Kicheche usikae uchi,huku umevaa sketi ya ngoma.
Safisha kope,braza mungu sio deusi.
We hushangai mzungu mweupe,ila ana kivuli cheusi.
Kuitwa lijali,ina maana nyumbani tule.
Ukimwi kuutibu aghali,sasa iweje uupate kwa bure.
Binti usitoe mimba,ukihisi utakosa soko.
Zaa umtunze kinda,mbinguni usichomwe moto.
Acha kuiba,we fisadi uliyetukuka.
Mstue na ngariba,nae aache watu wanakufa.
Dogo unayekunywa gongo,ukifa utazikwa la mboto.
Na denti skuli ndo mchongo,ya mjomba mwachie mpoto.
Teja pandisha mlege,rudisha kete kwa pusha.
Mwambie atanyea debe,akikamatwa na vya arusha.
Acha makuzi,mpendaji ili ufike mbali.
Mapenzi king’amuzi,na pesa ndo digitali.

Choruss (darassa&warda)
Vipi umekaa, chini,na muda unakwenda mbio./
Kwenye nchi masikini,na  wingi wa matukio./
Waambie jamaa,huu ni mwendelezo sio ujio./
Niko na kitu cha kusema,nipe muda na sikio./
Ukiwa mtaani,hizi ripoti(mwambie mwenzio)
Au umechill masikani jirani(mwambie mwenzio)
Mfanyakazi au mkulima shambani(mwambie mwenzio)
Mwanafunzi na mitaa huu ujumbe(mwambie mwenzio)

Vers 2(Stamina)
Ewe mtegemea ndugu,mwenye mikono na miguu.
Umasikini tatizo sugu,kuliko hata mr II.
Baba la baba,weka ubaba kila level.
Kitaani usawa unakaba,hadi padri anaishi kwa devil.
Mabadiliko,daima huanza na wewe.
Kama unakokwenda siko,uliza ili usichelewe.
Mche mungu,kama hajapanga hajapanga.
Kama ridhiki mafungu,kwanini ushinde kwa mganga.
Kusoma mpaka uchizi,ni kukosa kujiamini.
Mvivu unayependa usingizi,utakufa ukiwa masikini.
Endapo utailaza akili,usitegemee shida kukuamsha.
Hakuna mpenzi kama dili,funga nae pingu za maisha.
Hakuna tofauti,kati ya tajiri na masikini.
Uvae bukta uvae suti,ila wote tutazikwa chini.
Msimtenge mkiwa,kisa wazazi wake walimtupa.
Hata ng’ombe ana maziwa,ila akila simu anakufa.

Choruss (darassa&warda)
Vipi umekaa, chini,na muda unakwenda mbio./
Kwenye nchi masikini,na  wingi wa matukio./
Waambie jamaa,huu ni mwendelezo sio ujio./
Niko na kitu cha kusema,nipe muda na sikio./
Ukiwa mtaani,hizi ripoti(mwambie mwenzio)
Au umechill masikani jirani(mwambie mwenzio)
Mfanyakazi au mkulima shambani(mwambie mwenzio)
Mwanafunzi na mitaa huu ujumbe(mwambie mwenzio)

Vers 3(Stamina)
Huna hata cheti cha form 4,na una ndoto za kuwa raisi.
Nyumbani unajaza choo,hupaswi kungoja na urithi.
Kufeli hasara,akili hailetwi na milo.
Sio kisa dunia duara,ndo denti upate ziro.
Kila kitu kizuri,duniani huletwa na pesa.
Kwanza elimu haina umri,usiogope kusoma memkwa.
Ujanja hauna miaka,kiujinga we baki mdogo.
Acha uchu wa madaraka,kwa kuongoza hadi vigogo.
Hivi vifo vya wasanii,vinatokea kama ajali.
Ee mungu mshushe nabii,atukumbushe kusali.
Tumia akili,maishani uongoze jahazi.
Na usitafute utajiri,kwa kumtoa kafara mzazi.
 hujachelewa bado,cha msingi we piga kago.
Shukuru bado unahema,wala usishushe vilago.
Kijana taifa la leo,usilale ijenge kesho.
Huu ukoloni mambo leo,usikufanye ujione special.
Choruss (darassa&warda)
Vipi umekaa, chini,na muda unakwenda mbio./
Kwenye nchi masikini,na  wingi wa matukio./
Waambie jamaa,huu ni mwendelezo sio ujio./
Niko na kitu cha kusema,nipe muda na sikio./
Ukiwa mtaani,hizi ripoti(mwambie mwenzio)
Au umechill masikani jirani(mwambie mwenzio)
Mfanyakazi au mkulima shambani(mwambie mwenzio)
Mwanafunzi na mitaa huu ujumbe(mwambie mwenzio)

Outro(warda)
Mwambie mwenzio (mwambie mwenzio)x4

20 comments:

Anonymous said...

Nice

Anonymous said...

tishaaaaaaaaaaaaa

Anonymous said...

Stamina atabaki kuwa STAMINA TU

Anonymous said...

umerudi VIZURI kijana

Anonymous said...

nimepanda chorus

Anonymous said...

bonge lakolabo ila mhhhh....Darasa nnomaaaaaaaaaa cjui kwann wanamnyma Tuzo -------from-David mlwilo ---irnga/mafinga...

Anonymous said...

bonge lakolabo ila mhhhh....Darasa nnomaaaaaaaaaa cjui kwann wanamnyma Tuzo -------from-David mlwilo ---irnga/mafinga...

Anonymous said...

Nyimboo mbovuu hamubadiliki wana hip hop wa bongo anae sifia au kama unajitumia comments mwenyewe ukweli wa mambo nyimboo mbayaa sanaa style hio hio mashairi ndo hayo hayoo nyimbo kiukweli wa mungu ni mbaya sanaa.

Anonymous said...

Kwel bro unamistar kwenzi....saluteee kwako!

Anonymous said...

Anatisha sana Stamina

Anonymous said...

safiii..tunahitaj mambo kama hayo,nyimbo zenye ujumbe safi kabisa..kazi nzuri STAMINA

Unknown said...

Umetisha kijana wendo utabaki wengine wote watapita

Unknown said...

Umetisha xna bro vijana tina elimika kupitia mistari kwenzi noma xna hii!b!!bbbbbbb!!!!!!!

UFUGAJI BORA WA KUKU TZ said...

Stamina nouma sana

Anonymous said...

Dah nouuuumaaaaaaaaa

Anonymous said...

Its a superb Track Congrats Stamina

Anonymous said...

Staman we yako mafumbo yani hapo akuna mstari wa mana ujui k2 fro ina kubeba

Anonymous said...

Stamina da 'Punch bway' keep on bringing de gud music

Anonymous said...

hakunaga kama stamina hapa bongo

dave wamalwa said...

yebo!! thats hiphop.salute stamina