22.11.13

Friday, July 19, 2013

(Lyrics) KAMA HUWEZI by RAMA DEE Feat LADY JAYDEE

Verse 1: JayDee

Vipi mpenzi huoni mbali
Kweli huwezi kwenda mbali, na mie
Kweli mengi huletwa ndani
Si halali kuyapokea yote unitupie
Tutagombana kila siku mpenzi
Tutaudhiana kila siku ndani
Tutatishana kugawana mali
Bila kumjua mchawi wetu nani



Chorus:
Kama huwezi
Kuwa mkweli
Kamwe mpenzi mbele hatutofika mama
Kama pesa, zipo za kututosha ma X2

Verse 2: Rama Dee

Hizi lawama ziishie leo leo
Isifikie wakwe wanivue vyeo
Kwa gubu lako tu, mamii
Lawama zako zisinitie uchizi
Nibadili mipango yetu mingi
Hatutagombana tukifata yetu
Hatutaudhiana tukipanga yetu
Hatutafikia kugawana mali, mimi na wee

Rudia Chorus x 2

Tutagombana kila siku mpenzi
Tutaudhiana kila siku ndani
Tutatishana kugawana mali
Bila kumjua mchawi wetu nani

Hatutagombana tukifata yetu
Hatutaudhiana tukipanga yetu
Hatutafikia kugawana mali
Mimi na we

Rudia chorus x 2

Song written by Rama Dee

Enjoy

3 comments:

Anonymous said...

coooool.......big up ramah

Anonymous said...

Bonge la traaaack....Bonge la kolabo....

Anonymous said...

Kama Wanaume Wote Wangezungumza Kama Rama dee kwenye verse Yake Kungekua hakuna malumbano ktk Mahusiano....Big uppppp