22.11.13

Tuesday, July 30, 2013

(News) Dk Bilal ahimiza Tehama kwa vijana

 Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal akipokea mifuko 30 ya saruji kutoka kwa Mwenyekiti wa Vodacom Foundatio Hassan Saleh ikiwa ni sehemu ya vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani ya Sh 10 Milioni vilivyotolewa na Vodacom kumalizia ujenzi wa kituo cha uendelezaji na ukuzaji matumizi ya Tehama cha Shule ya Msingi Kisiwandui. Wengine pichani kutoka kulia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni  Mahmoud Mohamed Mussa na Mbunge wa Jimbo hilo Masauni Hamad Masauni. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bi Taifa.

 Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal akipokea kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Masauni Hamad Masauni maelezo ya michoro ya ujenzi wa kituo cha ukuzaji na uendelezaji matumizi ya Tehama cha Shule ya Msingi Kikwajuni. Kushoto ni Mwenyekiti wa Vodacom Foundation Hassan Saleh ambae alimkabidhi Makamu wa Rais vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani ya Sh 10 Milioni kumalizia ujenzi wa kituo hicho.
 Mwenyekiti wa Vodacom Foundation Hassan Saleh akiongea na jumuiya ya Shule ya Msingi Kisiwandui wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya Sh. 10 Milioni vilivyotolewa na Vodacom kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha ukuzaji na uendelezaji matumizi ya Tehama cha Shule ya Misngi Kisiwandui Zanzibar. Vifaa hivyo vilikabidhiwa kwa Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal mwishoni mwa wiki Zanzibar.
Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal akipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Vodacom Foundation Hassan Saleh kompyuta kumi zenye thamani ya Sh 13 Milioni kwa ajili ya kusaidia kituo cha jamii cha mafunzo ya komyuta cha Chwaka Mjini Zanzibar. Makabidhiano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki Zanzibar.

Dk Bilal ahimiza Tehama kwa vijana
*    Asifu juhudi za Vodacom za kusaidia maendeleo
Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal ametoa rai ya kuongezwa kwa kasi ya uwekezaji wa elimu na uwezo wa matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano - Tehama kwa vijana nchini ili waweze kuishi kwenye enzi waliyomo inayotawaliwa na teknolojia..
Dk Bilal ametoa rai hiyo wakati akipokea msaada wa vifaa vya ujenzi kumalizia ujenzi wa kituo cha uendelezaji na ukuzaji matumizi ya Tehama cha Shule ya Msingi Kisiwandui pamoja na kompyuta kumi kwa ajili ya kituo cha kompyuta cha kijamii cha Chwaka vyote vya Mjini Zanzibar vilivyotolewa na Mfuko wa Kampuni ya Vodacom wa kusaidia jamii - Vodacom Foundation ambavyo kwa pamoja vina thamani ya Sh 23 Milioni.
Makamu wa Rais amesema uwekezaji kwenye Tehama ni moja ya mambo yanayopaswa kupewa kipaumbele kwa wakati huu hasa kwa vijana ambao hawana sababu ya kuishi nje ya mfumo na zama zinazotawaliwa na matumizi makubwa ya teknlojia katika kila Nyanja ya maisha ikiwemo mfumo rasmi wa elimu.
Amesema maisha ya sasa yanahitaji kompyuta na Tehama kwa kiaisi kikubwa na hivyo kuipongeza Vodacom Foundation kwa kuona umuhimu wa kusaidia vituo hivyo viwili msaada ambao ni wa wakati na wa umuhimu kulingana na mahitaji ya wakati.
"Viongozi wa ngazi zote za serikali tuweke ajenda ya Tehama ili kuviwezesha vizazi vya sasa kuishi na wakati wao."Alisema Dk Bilal na kuongeza kuwa "Sisi tuliozaliwa na kukulia katika zama za BBC(Born Before Computer) tunapoona mapinduzi haya makubwa ya kiteknolojia tunakumbuka tulipotoka na tunawaza ni vipi maisha yatakuwa katika miaka michache ijayo kutokana na ukuaji wa kasi wa matumizi ya Tehama."Alisema Makamu wa Rais Dk Bilal.
"Tunachotaka ni kuona vijana ambao ndio wa kizazi cha Tehama wasiulize wanachokitaka leo bali wajiulize na kupata suluhu ya nini kitakachohitajika miaka ijayo na ili tufikie huko ni lazima tuwaandae vijana na tuwekeze kisawaswa kwenye Tehama na kutokana na hilo basi ndio maana nawashukuru sana Vodacom kwa kuona umuhumi wa Tehama kwa jamii na kutoa misaada hii."Aliongeza Dk Bilal katika hafla hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki Mjini Zanzibar Amesema vituo hivyo vitawasaidia sana vijana kujifunza mambo ambayo hawajayasoma darasani  kupata uelewa na ufahamu wa mambo ambayo hawajawahi kuyafahamu.
"Kila kitu siku hizi kipo kwenye mtandao hakuna haja ya kusumbuka kama ilivyokuwa wakati wetu ambapo Mwalimu kwa mfano alilazimika kutumia muda mwingi sana kusoma kitabu kizima ili kupata notisi za kufundishia darasani, lakini sasa kila kitu ni kudadavua tu."
Dk Bilal ambae alitumia muda mwingi kuelezea utofauti wa maisha yalivyokuwa enzi za bila ya kompyuta na hali ilivyo hivi sasa amewaomba wadau wengi zaidi kujitokeza na kusiadia juhudi za ukuzaji na uendelzaji wa matumizi ya Tehama kwa vijana ili kwualinda vijana hao kutosihi kizamani.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Vodacom Foundation Hassan Saleh amesema muono wa Vodacom ni kuona kila mtanzania anafikiwa kwa urahisi na huduma za Intaneti ili kuweza kunufaika na mapinduzi ya kiteknolojia yanayotoeka ulimwenguni.
"Nia ya kampuni ya Vodacom ni kuona kila Mtanzania anafikiwa na huduma za Intaneti na kuwa na uwezo wa kuzitumia kwa kuwa tunatambua umuhimu wake kwa maisha ya watu na maendeleo yao kwa sasa bila kujali aina ya kazi au  kipato, na ndio maana tumejitoa kusiadia vituo hivi vinavyoleta huduma za Tehama karibu na watu." 
Saleh amesema Vodacom Foundation imekuwa karibu na jamii kwa kusaidia ustawi wa maendeleo ya jamii hasa katika maeno ya elimu, afya na ustawi wa jamii kwa kutambua na kuunga mkono juhudi za serikali zinazofanywa katika kuleta maendeleo.
"Tumekuwa tukifanya uwekezaji mkubwa kwa jamii yote hii ni kuunga mkono juhudi za dhati zinazofanywa na serikali zote mbili ya Muungano na ya Zanzibar katika kutatua changamoto mbalimbali za kijamii."Alisema Saleh na kuongeza "Azima yetu ya kusaidia jamii bado ipo imara na tunaedela nayo."
Sale ameongeza kuwa hata misaada hiyo ni kielelezo na mwendelezo wa mchango wa Vodacom katika maendeleo ya wananchi ikitambua na kuheshmu mchango wa jamii inamofanyia biashara kwenye maendeleo ya kibiashara ya kampuni yake.
Mwisho.

No comments: