22.11.13

Saturday, July 06, 2013

(News) Oxford na Vodacom zaungana kuendeleza Elimu nchini

 Meneja  Mauzo na Masoko wa Oxford University Press Bi.Fatma Shangazi(kulia)akimuonesha Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu (kushoto) na Meneja maendeleo ya kibiashara wa kampuni hiyo Asia Mhina, moja ya vitabu vinavyouzwa kwenye  banda lao katika viwanja vya maonesho ya 37 ya  biashara ya kimataifa (sabasaba) wakati wa uzinduzi wa ushirikiano baina ya kampuni yake na Vodacom utakao wawezesha wateja kutumia huduma ya M PESA kununua vitabu.

 Meneja maendeleo ya kibiashara wa kampuni ya Oxford University Press,  Asia Mhina (kushoto) na  Meneja  Mauzo na Masoko wa kamnpunoi hiyo Bi.Fatma Shangazi(kulia)wakifatilia neno kutoka kwa Meneja wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu katika moja ya Kamusi ”Dictionary” zinazouzwa kwenye  banda lao katika viwanja vya maonesho ya 37 ya  biashara ya kimataifa (sabasaba) wakati wa uzinduzi wa ushirikiano baina ya kampuni yake na Vodacom utakao wawezesha wateja kutumia huduma ya M PESA kununua vitabu.

Meneja  Mauzo na Masoko wa Oxford University Bi.Fatma Shangazi(kulia)akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) moja ya vitabu vinavyouzwa kwenye  banda lao katika viwanja vya maonesho ya 37 ya  biashara ya kimataifa (sabasaba) wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya kampuni yake na Vodacom utakao wawezesha wateja wanaotumia huduma ya M PESA kununua vitabu, wanaoshuhudia kutoka kushoto ni  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu na  Meneja maendeleo ya kibiashara wa kampuni hiyo Asia Mhina.

Ili kuongeza kasi ya usomaji wa vitabu kwa watanzania suala ambalo limekuwa ni changamoto kubwa hapa nchini  kampuni ya Oxford University Press imeingia ubia na Vodacom Tanzania ili kuwawezesha wateja mbalimbali kununua vitabu kupitia huduma ya M pesa, Vitabu vitakavyo weza kununuliwa na kuuzwa ni pamoja na vile vya kiada na Ziada kutoka katika kampuni hiyo.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Ushirikiano huo  uliofanyika katika maonesho ya 37 ya Sabasaba Meneja Ukuzaji Biashara wa Vodacom Asia  Mhina amesema kuwa kutokana na kukua zaidi kwa huduma ya  M-Pesa hapa nchini pamoja na kuepuka usambazaji kwa wateja wa Oxford ndiyo sababu iliyosababisha wao kuingia ubia huo.
Mhina alibainisha pia ubia huo umekuja katika wakati muafaka kwa ajili ya kuwarahisishia wateja wa vitabu kuepukana na foleni zilizopo kwenye mabenki pamoja na kuokoa muda wa malipo kwa wateja pia kuongeza kasi ya ununuaji na usomaji wa vitabu kwa Watanzania.
“Lengo la huduma hii ni kuwarahisishia wateja na wananchi kufanya malipo ya vitabu kwa urahisi , pia kuongeza kasi ya ununuaji na usomaji wa vitabu kwa Watanzania suala ambalo limekuwa ni changamoto kubwa sasa, hivyo hatua hii itawezesha kukabiliana na changamoto hizo,” alisema Mhina na kuongeza kuwa,
“Mteja wa Vodacom sasa atalipia vitabu hivyo kwa njia rahisi zaidi ambapo akitaka kufanya malipo atafungua orodha ya M pesa kama kawaida na kisha kuchagua malipo na kuweka namba ya biashara ya Oxford ambayo ni 870870 na kisha kufanya malipo.”
Kwa upande wake meneja masoko wa Oxford   Fatma Shangazi alisema kuwa  huduma ya malipo ya vitabu kwa M-Pesa itawarahisishia wateja wao kufanya malipo kwa urahisi pasipo usumbufu wowote wala kupoteza muda na pia itawaweka katika hali ya usalama zaidi.
“Tunafurahi kuingia katika ubia na kampuni ya Vodacom ni hatua kubwa kwetu na tunaamini kuwa ushirikiano huu utakuwa chachu ya kuongeza hali ya usomaji wa vitabu kwa Watanzania, alisema Shangazi.
MWISHO

No comments: