22.11.13

Tuesday, July 09, 2013

(News) TECNO kuwekeza zaidi katika soko laTanzania

 Meneja Mauzo wa kampuni ya uuzaji wa simu za mkononi  aina ya TECNO, Patrick Karogila, akionyesha moja ya simu za teknolojia ya hali ya juu “Smartphone” ambayo imeingizwa katika soko la Tanzania hivi karibuni, Simu hiyo pamoja na nyingine zimebuniwa ili kukidhi mahitaji ya watumiaji wa simu nchini, pamoja nae ni Afisa Uhusiano wa kampuni hiyo Boukali Mounir.

 Meneja Uhusiano wa kampuni ya uuzaji wa simu za mkononi aina ya TECNO, akionyesha moja ya simu zenye teknolojia ya hali ya juu “Smartphones” ambayo imeingizwa katika soko la Tanzania hivi karibuni, Simu hiyo imebuniwa kukidhi mahitaji ya mawasiliano kwa watumiaji wa simu nchini, pamoja nae ni Meneja Mauzo wa kampuni hiyo Patrick Karogila.

Meneja Mauzo wa kampuni ya uuzaji wa simu za mkononi  aina ya TECNO, Patrick Karogila, akizungumza na waandishi wa habari, (hawapo pichani) katika hafla ya kutambulisha simu zilizotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu kutoka katika kampuni hiyo, Simu hizo zimebuniwa kukidhi mahitaji ya mawasiliano kwa Watanzania wa aina zote. Pamoja nae ni meneja mahusiano wa kampuni hiyo, Boukali Mounir.

Dar es Salaam, Tanzania Julai 7, 2013 Kampuni ya uuzaji wa simu za mkononi ya TECNO imeendelea kuwekeza zaidi katika soko la Tanzania ili kukidhi haja ya mawasiliano na ajira kwa watanzania ikiwa ni sehemu ya matunda ya ushirikiano mzuri kati ya nchi ya Tanzania na China.
Kukua kwa uwekezaji wa kampuni hiyo kwa kasi katika siku za karibuni kumefuatana na utengenezwaji wa simu za teknolojia ya hali ya juu “Smartphones” ambapo sasa kampuni hiyo inazitengeneza na kuuzwa katika soko la nchi mbalimbali barani Afrika ikiwemo Tanzania kwa bei nafuu.
Pamoja na simu nyingine za teknolojia ya hali ya juu, simu mpya ambayo imeingizwa katika soko ni aina ya TECNO P3 ambayo imetengenezwa kukidhi mahitaji ya watumiaji kwa kuwa na teknolojia ya hali ya juu ya mawasiliano iliyowezeshwa kwa teknolojia ya Android 2.3 na kuiweza kufanya kazi sawa na  simu za teknolojia ya juu yaani Smartphones.
Kwa kutumia simu hiyo ya P 3 wateja wataweza kupata uwezo mzuri wa kutumia internet kwa kasi ya hali ya juu pamoja na kuunganishwa na mitandao mablimbali ya kijamii, hususani kwa watanzania wa kada ya chini na wale wa vijijini abao matumizi ya intanet kwao imekuwa changamoto kubwa.
Kampuni hiyo ambayo imeendelea kujiimarisha katika soko la Tanzania kwa kuanzisha uuzwaji wa simu za teknolojia ya juu inatarajia kuingia katika ushirikiano na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom katika kuwawezesha watanzania zaidi kufurahia mawasiliano.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Meneja mahusiano wa kampuni ya TECNO, Mounir Boukali amesema, “ Tunatambua kuwa idadi kubwa ya watanzania wanauhitaji wa kutumia simu zenye teknolojia ya hali ya juu na yenye uwezo wa kuwa na intanet yenye kasi, matarajio haya hakika yanaletwa na simu hii ya TECNO P3 ambayo tumeiingiza sokoni punde.
Mounir alifafanua zaidi kuwa kampuni yake pia imeingiza katika soko aina nyingine ya Smartphones ambazo zinauzwa kwa bei ambayo watanzania wengi wanaweza  kuimudu.
 “Soko la mawasiliano na simu limeshuhudia ongezeko kubwa la matumizi ya intanet katika nyanja mbalimbali, hivyo ni wakati muafaka kwa makampuni ya simu na watengenezaji wa simu kuungana pamoja katika kuhakikisha wanakidhi mahitaji ya wateja wao,”
Akizungumzia simu hiyo Mounir alisema, TECNO P3 ina kioo cha kushika kwa mkono ( Touch screen) pia ina Wi – Fi, na imeunganishwa na huduma ya Facebook, Google Play Store, Gmail , Yahoo , Opera Mini, Whatsup na nyinginezo, na la muhimu zaidi ni kwamba simu hiyo ina laini mbili za simu.
Pamoja na kujiimarisha huko katika soko la biashara kampuni hiyo pia imeendelea kujenga ajira kwa watanzania ikiwa ni sehemu mojawapo ya faida za uwekezaji wa kampuni hiyo nchini.
Dunia ya sasa imeshuhudia mapinduzi makubwa ya kiteknolojia ambapo nchi zinazoendelea zinahitaji maendeleo haya katika kuhakikisha zinaendana na kasi ya maendeleo kulingana na teknolojia hiyo katika kufikia malengo yao ya kiuchumi na kijamii.

No comments: