22.11.13

Thursday, August 29, 2013

(Audio) Bosco Baya - Urafiki wa MPesa

       Bosco Baya ni mzaliwa wa pwani ya Kenya na msanii  wa  mziki wa kizazi kipya.Anafahamika kwa miondoko ya kivyake ,uimbaji wake na staili anayotumia kwa uwasilishaji ujumbe ni wenye hisia na unaogusa.Alisomea shule ya upili ya Mt.Terezia, iliyo kaunti ya kilifi alikozaliwa.

     Amelelewa na Mama yake kwa shida na raha….anadai kumpenda sana mama yake kuliko chochote kile.Kijana huyu mcheshi mwenye miaka ishirini na nne yuko katika mikataba na kituo cha kurekodi cha Kusini Rekodi Kilicho kati kati mwa jiji la Nairobi.
   Alianza mziki rasmi miaka ya 2005 ,akiwa kidato cha pili.Alizinduliwa na Tino The Don producer anayezindua na kukuza vipaji nnchini Kenya kaunti ya kilifi.Aliingia studioni 2006 na kupata kurekodiwa na Producer aliyemahiri na aliyeboboea kwa mitindo ya hiphop,ragga,reggae  na rnb.Producer huyu Edward Ananda anayejulikana kama Ananda1 ndiye aliyembadilisha Bosco baya kutoka kwa mitindo ya hiphop hadi akawa mwimbaji mahiri sana wa mitindo ya Afrofussion.
    Ametambulika na kibao chake Barua aina ya rhumba kilicho chezwa na kurekodiwa Kusini Records na maproducer Black Child and Ananda.Kibao hicho kilicho vuma Kenya nzima kimempa sifa zote bwana huyo.Anavibao vinavyotikisa kama Urafiki wa M-Pesa ,Siku njema na vingi vyengine.Nimkaazi wa jiji la Nairobi na mpishi wa mikate na keki.

No comments: