22.11.13

Monday, August 19, 2013

(Freedom of Speech) DUDUBAYA: WASANII WA BONGO WAMEZUNGUKWA NA WAPAMBE NA SIO MARAFIKI

 Dudubaya

Dudubaya leo amezungumza na DJCHOKAblog na kusema yake yaliyoko moyoni bila kumuogopa mtu yoyote, namnukuu

"Wasanii wa bongo wamezungukwa na wapambe na siyo marafiki, mpambe ni mtu asiyeweza kukushauri maendeleo, wao ushauri wao ni starehe. Rafiki ni mtu anayekupenda anayekutakia mema na mshauri wa maendeleo hata wakati wa shida utakuwa nae."

Dudubaya hakusita kusema tena vitu vingine ambavyo vinamkwanza kwa sasa hivi... Namnukuu

"South Africa, West Africa wanatoboa kwasababu media zina love na wasanii wao, bongo tunasusmbuliwa na wivu roho mbaya, that why hatusongi mbelr. Muziki wa bongo unapendwa nchi nyingi ila mipaka ya mafanikio zimefungwa. Wanainua wasanii wapya si nia nzuri bali kwa manufaa yao. Maana hawa makinda bado akili zao ndogo, wanawatumia then wanawaacha wanaangukia matako, wadau hawapo kwa ajili ya kuwapeleka wasanii kimataifa" 

Dudubaya (Mamba)

1 comment:

japhet james said...

Dudubaya uko sawa kabisa, wasanii wetu wameshikwa sana masikio na wanaojiita wadau wa muziki.