22.11.13

Thursday, August 15, 2013

(News) BABU TALE asema yuko tayari kumpokea DOGO JANJA TIP TOP hata leo.....

Babu Tale
Imeonekana kama drama flani hivi na kuchukuliwa kama Story ya kimya kimya flani hivi ila kwa sasa imekuwa wazo kupitia DJ HAAZU wa MJ Radio ARUSHA ambaye ameamua kuziunganisha sauti za Vichwa Vitatu ambavyo ni Janjaro, Madee na Babu Tale.

Madee & Janjaro
 
Ni juzi juzi tu ambapo Manager wa kundi la TipTop Connection Babu Tale alifunguka kuwa Dogo Janja anampigia magoti Madee kuwa wamrudishe TipTop na hapa ikabidi Haazu apate sauti za Wahusika wote kupitia MJ RADIO ambapo alimpigia simu Babu Tale ambaye alithibitisha hilo na kuonekana wazi kuwa anatamani Dogo janja Arudi TipTop Connection huku akijilinda na kile alichokiita kuwa yeye na Janjaro zinaiva na hajawahi kugombana na Dogo janja.
Msikilize Babu Tale hapa chini akimthibitishia Haazu kuwa yuko tayari Dogo Janja arudi TipTop
 
CLICK HAPA
http://www.hulkshare.com/36w6jwd09xa8
DJ HAAZU alipotamani kujua kutoka kwa Tale kuwa labda alijisikia vibaya kipindi ambacho Dogo alitoka TipTop yeye Tale alijibu kuwa hakujiskia Vibaya kwani ni Maisha aliyokuwa ameamua Dogo ila ukweli umesimama.
msikilize Tale hapo chini tena....

CLICK HAPA
http://www.hulkshare.com/tvh0cxnmb9c0

Kwa upande wa story za kitaa zinazodai kuwa Manager wa Mtanashati ent....Ostaz Juma Namusoma amefulia bado hatujazithibitisha Ila kwa Upande wa Babu Tale alipoulizwa kuwa Janjaro alibug kwenda Mtanashati alijibu kama anauma anapuliza......
Msikilize Tena Tale hapo Chini.

CLICK HAPA
http://www.hulkshare.com/5fzk2yk6m22o

DOGO JANJA YEYE ANASEMA BADO YUKO MTANASHATI
Kingine hawezi kubishana na bob Tale

MSIKIZE JANJARO HAPA CHINI

CLICK HAPA
http://www.hulkshare.com/bh7o28n22olc

LAKINI JE KUHUSU JANJARO YUKO TAYARI KURUDI TIPTOP?????

Hilo ndilo lilikuwa swali la pili la DJ HAAZU kwa Dogo Janja ambapo yeye alijibu kuwa yuko tayari kurudi ila kwa Maelewano ya maana kuhusu kulindiwa na kupewa haki yake inavyostahili na sio mapichapicha.
Msikilize Janjaro hapo chini akifunguka
CLICK HAPA
http://www.hulkshare.com/52akv9pxeark

VITU ANAVYOTAKA VIWEKWE SAWA ILI ARUDI TIPTOP
ALIVITAJA MSIKILIZE HAPA
http://www.hulkshare.com/uhvgmahc7klc

DOGO JANJA ANAJUA OSTAZ KAFULIA?
Hili lilimuhusu pia Janjaro ambapo yeye alijibu kuwa kuna wakati mtu anayumba kiasi flani ila hawezi Msemea Ostaz kwani atakuwa anaingilia Uhuru wa mtu Binafsi.

Msikilize tena hapa Janjaro akifunguka kuhusu Kesi ya kuwa Boss wake Kafua
CLICK HAPA
http://www.hulkshare.com/7piieo4qs9og


JE MADEE YEYE ANASEMAJE...?
DJ HAAZU akataka kujua kama Raisi wa TIpTop Madee ambaye yeye ndiye aliyekuwa ametajwa na Janjaro kama mhalifu wake wakati anatoka TipTop Je atakuwa ameyamaliza na janjaro?, ambapo Madee yeye amesema alishamsamehe Dogo kitambo sana na akamwambia kabisa kuwa amemsamehe na kwamba wanaongeaga na Janjaro kama Mdogo wake na kusema kuwa alijua ni watu waliokuwa wanataka kumuharibia future janjaro ila kwa sasa ukweli umesimama na yeye toka kipindi kile alimchukulia Dogo kama mtoto na ndio maana akatekwa  kirahisi ila kwa sasa Dogo Kajua ukweli na yeye Madee kuthibitisha kuwa hakumlaumu Dogo
 
MSIKILIZE MADEE HAPO CHINI AKIFUNGUKA

CLICK HAPA
http://www.hulkshare.com/291n9gba1n4w

 MADEE AMESHAMWAMBIA JANJARO KUWA AMEMSAMEHE MSIKIE TENA HAPO CHINI

CLICK HAPA
http://www.hulkshare.com/291n9gba1n4w

HIYO NDO HABARI KAMILI KWA SASA KAMA OSTAADHI KAFULIA KWELI BASI ENDELEA KUFUATILIA STORY ZETU HAPA HAPA.

STORY BY DJ HAAZU

No comments: