22.11.13

Tuesday, August 06, 2013

(News) BENKI YA KCB YATOA MISAADA YENYE THAMANI YA SHILINGI TSH 7,200,000 KWA HOSPITALI YA MWANANYAMALA NA KUAIDI KUFANYA MAKUBWA SEKTA YA ELIMU NCHINI

 Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala, Dk.Sophinias Ngonyani (kushoto), akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa vifaa tiba vya kuwekea mgonjwa gesi, vilivyotolewa na benki ya KCB kwa hospitali hiyo, Dar es Salaam jana. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KCB, Godfrey Ndalahwa na katikati ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye.

 Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye, akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala, Dk. Sophinias Ngonyani (kushoto), moja ya vifaa tiba vyenye thamani ya sh. milioni 7.2, vilivyotolewa na benki hiyo, vinavyotumika kwa ajili ya kumwekea gesi mgonjwa, Dar es Salaam jana. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KCB, Godfrey Ndalahwa.
 Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala, Dk. Sophinias Ngonyani, akiangalia moja ya vifaa tiba vya kumwekea mgonjwa gesi, mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye (katikati), vifaa vilivyotolewa na benki hiyo kwa hospitali hiyo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KCB, Godfrey Ndalahwa.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB, Godfrey Ndalahwa, akimkabidhi moja ya boksi lenye vifaa vya kumwekea mgonjwa gesi, Mkuu wa Bima ya Afya wa Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala, Dk. Merina Nkullua, vilivyotolewa na benki hiyo, Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye.
 Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Oysterbay, Gladys Mhina, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya benki ya KCB, kuchangia madawati inayoitwa 'Buy 10 Get 90, ambayo benki hiyo itanunua madawati 90 na shule husika kutakiwa kununua madawati 10. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB, Godfrey Ndalahwa na katikati ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye.

No comments: