Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania
Rene
Meza, akizungumza na waandishi wa habari, (hawapo pichani) kuhusiana na
kurejeshwa kwa huduma zote za mtandao wa Vodacom baada ya kukosekana kwa
saa 16
kufuatia moto kuzuka katika kitovu cha kuendeshea mitambo jijini Dar es
Salaam,Mkutano huo ulifanyika katika hoteli ya Serena Jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene
Meza, akizungumza na waandishi wa habari, (hawapo pichani) kuhusiana na
kurejeshwa kwa huduma za mtandao wa Vodacom baada ya kukosekana kwa saa 16
kufuatia moto kuzuka katika kitovu cha kuendeshea mitambo jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo ulifanyika katika hoteli ya Serena,Pamoja nae ni Mkuu wa kitengo
cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa.
Taarifa kwa vyombo vya habari
Huduma ya Mawasiliano ya Vodacom yarejeshwa.
· Ni Baada ya moto kuungunza
mitambo
· Mtandao ulizimwa kwa saa 16 nchi
nzima
Dar es Salaam, Agosti 18, 2013 ……. Baada ya
kukosekana kwa huduma za mtandao wa Vodacom kwa takribani masaa 16, huduma hizo
zimerejeshwa katika hali yake ya kawaida asubuhi ya Jumamosi ya Agosti 17.
Akizungumzia tatizo
lililosababisha kukosekana kwa huduma za mawasiliano kwa watumiaji wa mtandao
huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza amesema chanzo cha
kukatika kwa mawasiliano nchi nzima siku ya Ijumaa ni moto uliotokea katika mtambo
mkuu wa kuendeshea mtandao (Main Switch) uliyoko Dar es Salaam.
“Kufuatia hatua hiyo, hatukuwa tena na uwezo
wa kutoa huduma kwa watu wote kuanzia siku ya Ijumaa jioni hadi Jumamosi
asubuhi, hali hii iliathiri wateja wetu wote kwa ujumla kwani walishindwa
kuwasiliana na ndugu jamaa na marafiki ambao wote ni wateja wetu, alisema Meza.
Aidha aliomba radhi kwa
jamii ya Watanzania na wateja wa Mtandao wa Vodacom kwa kukosa mawasiliano
katika kipindi hicho, na kusema kuwa wateja wote wa mtandao wa Vodacom watarudishiwa
gharama zote kwa huduma yoyote walionunua na kuhitaji kuitumia wakati ambapo
mtandao haukuwa unapatikana, “Fidia hizi
kwa wateja wetu wote zitatolewa siku ya jumatatu ya Agosti 19, 2013 alisema
Meza.
“Tunaishi katika dunia ambayo mawasiliano ni
muhimu katika maisha yetu ya kila siku hivyo tunaelewa kuwa tatizo hili
limekuwa kikwazo kikubwa kwa wateja wetu, Na tunawashukuru kwa kuwa waelewa na
wavumilivu katika kipindi chote ambacho tumekuwa tukikabiliana na tatizo hili,
alisema Meza.
Meza alihitimisha kwa
kuhakakikishia Watanzania na wateja wa Vodacom kwa ujumla kuwa Vodacom imedhamiria
kuendelea kutoa huduma zenye viwango vya hali ya juu nchini.
“Ninapenda kuwashukuru wafanyakazi wetu wote
na washirika wetu ambao kwa pamoja wamefanya kazi bila kuchoka katika
kuhakikisha huduma zote zinarejea hadi katika hali ya kawaida hadi kufikia Jumamosi
asubuhi, Jitihada zao na kazi kubwa waliyoifanya imewezesha huduma zote kurejea
katika hali ya kawaida, alihitimisha Meza.
Mwisho………
No comments:
Post a Comment