22.11.13

Friday, August 09, 2013

(News) Jose Chameleon kupagawisha Dar Escape Complex Eid Pili

Mwanamuziki kutoka Uganda, Dr. Jose Chameleon anatarajiwa kufanya onyesho kali kesho kwenye ukumbi mpya wa burudani wa Escape Complex.

Chameleon, ambaye ndie mwanamuziki mashuhuri kuliko wote kwenye ukanda huu wa Afrrika Mashariki anatarajiwa kukonga nyoyo za wakazi wa Dar es Salaam kwa kuimba nyimbo zake zote kali, ikiwemo Valuvalu.
 
Usiku huo wa Chameleon utaenda sambamba na burudani kali kutoka kwa MA DJ wakali, DJ Pac na DJ Senorita ambao watafanya show ya utangulizi.

Akizungumzia burudani hizo, Meneja Uendelezi wa Biashara wa Escape Complex, Anthony David, alisema watu watarajie burudani kali siku ya jumamosi hasa kwa kuwa sherehe hizo zitaenda sambamba na sherehe za Eid za pale Escape Complex.

‘Kama lilivyo jina lake, Escape ni mahali ambapo mtu anakuja kupumzika kukwepa mihangaiko ya kila siku, iwe kikazi au kimaisha, lakini Eid hii tumeandaa burudani hii ili kuwapa wakazi wa Dar es Salaam kitu tofauti’ anasema Anthony.

Mbali na Chameleon siku ya jumamosi, Escape Complex imeandaa burudani siku ya Eid Mosi, ambapo DJ maarufu Boni Luv atatoa burudani kali, na siku ya Jumpili, bendi inayokuja kwa kasi Skylight, itawaburudisha wapenzi wake kuanzia asubuhi ili kuimaliza wikiendi ndefu.

Escape Complex, ambayo ipo Mikocheni/Kawe karibu nyuma ya ukumbi wa Safari Carnival, ni Club mpya ambayo inapendezeshwa na ufukwe pamoja na mandhari ya kuvutia, pamoja na chakula kizuri kwa wateja wake.

Mashabiki wa Chameleon watalipia shilingi elfu kumi na tano ili kuburudishwa na mwanamuziki huyo mashuhuri. Na VIP watalipa elfu 40,000/= ikiwemo kinywaji cha bure pamoja na nafasi ya kumuona msanii huyo baada ya maonyesho.

No comments: