22.11.13

Thursday, August 29, 2013

(News) Kova awatahadharisha wananchi kutokubeba fedha nyingi

Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Suleiman Kova,akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na Watanzania kuacha utamaduni wa kubeba pesa nyingi badala yake watumie mfumo wa kielektroniki wa M-PESA kwani ni sehemu ya maisha ya mtanzania kwa sasa,wengine kutoka kushoto ni wafanyakazi wa Vodacom Tanzania.
Dar es Salaam, 29 Agosti, 2013 ... Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Suleiman Kova, amewataka wananchi wenye mazoea ya kubeba fedha nyingi kutoka sehemu moja kwenda nyingine kuacha tabia hiyo kutokana na sababu za kiusalama.
Kamishina Kova ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi kuu za polisi kanda maalum ya Dar es Salaam huku akitanabaisha kuongezeka kwa matukio ya watu kuporwa fedha wakiwa wanaelekea au wanatoka katika mabenki na wakati mwingine kutokea kwa vifo.
"Jeshi la polisi linafanya jitihada kubwa kukabiliana na uhalifu wa aina mbalimbali, tunataka wananchi watupe ushirikiano ili tuweze kupunguza matukio ya uhalifu, Kazi kubwa ya polisi ni kuzuia uhalifu na sio kupambana na uhalifu hivyo wananchi wanatakiwa wawe wa kwanza kuzuia uharifu usitokee". Alisema Kova na kuongeza.
"Kwa wadau mbali mbali katika kuhakikisha usalama wa raia wa nchi leo tunayofuraha kushirikiana na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom kupitia huduma ya M pesa katika kuleta suluhisho la uvamizi kwa watu wenye mazoea yakubeba fedha nyingi kutoka sehemu moja kwenda nyingine,"
Alisema kuwa kuna watu wanadhani kuwa na fedha nyingi ndani au kubeba fedha nyingi ni ufahari, "Kuna watu wanatabia za kushangaza sana, mtu anafurahi kubeba pesa nyingi  akijiona ni ufahari na hata wakati mwingine kuwaita watu na kuwaonyesha pesa zao ili wawaogope au kuwasifia utamaduni huo umepitwa na wakati."
Kova alisema jamii ya sasa inatakiwa kutoka katika mfumo wa matumizi ya fedha taslim, (Cash Sosiety) na kuwa jamii yenye matumizi ya fedha kwa njia za Ki elektroniki (Cashless Society) Ili kuokoa trasilimali za jeshi la polisi na vifo visivyo vya lazima kwa askari au raia.
"Katika usindikizwaji na polisi kunaweza kukatokea uvamizi ambao unaweza kuleta mapambano na hatimaye kusababisha vifo, "Nawasihi wote mtumie mfumo huu maalum wa M pesa katika kuhifadhi pesa zenu na katika kuwalipia wafanyakazi mishahara yao na hata magawio mengine kwasababu ndio njia yenye usalama zaidi kuliko kutoa fedha benki na kutembea nazo. Kwa kufanya hivyo mtakuwa mmelisaidia jeshi la polisi katika operesheni zake kwasababu ni mfumo wa kiusalama zaidi hivyo kupelekea uhalifu kupungua na kutupunguzia sisi gharama za operesheni zetu katika kuhakikisha usalama wa wananchi."
Kwa upande wake Mkuu wa Ukuzaji wa Biashara M-Pesa, Jackson Kiswaga alifafanua zaidi mfumo huo unaotumia M-Pesa kufanya kazi.
"Mfumo huu mpya wa kielektroniki wa kulipa mishahara na magawio kwa njia ya M-Pesa ni rahisi na ya haraka zaidi. Kitakachofanyika hela zitatumwa kutoka akaunti yako ya benki kwenda kwenye akaunti inayoitwa Fast Account ambayo ni ya M- Pesa alafu kwenda kwenye akaunti ya kawaida ya M-Pesa na hapo ndipo unaweza kulipa wafanyakazi wako kwa kuandika tu majina yao nambari zao za simu na kiasi kisha kubonyeza kitufe cha kutumia," alisema Kiswaga.
Alimalizia kwa kusema kuwa kwa mfumo huu unaweza kulipa wafanyakazi zaidi ya mia mbili kwa wakati moja na vilviele kwa wafanyabiashara wanaoingiza zaidi ya billioni moja wanaweza wakajiunga na M-Pesa daraja la tatu (level three)  na kujiwekea fedha zao kwenye akaunti ya M-Pesa na ataweza kulipa shilingi milioni kumi na mbili kwa wakati mmoja na milioni 50 kwa siku.
Mwisho .......

No comments: