22.11.13

Monday, August 12, 2013

(News) MASHINDANO YA MIJADALA YA SHULE ZA SEKONDARI MWANZA KUANZA SEPT. 2.

Mashindano ya Mijadala kwa shule za sekondari mkoani Mwanza (Interschools Debate Competition), yanatarajiwa kuanza septemba 02 mwaka huu.
Akizungumza katika semina elekezi, iliyowakutanisha baadhi ya walimu wa mijadala kutoka katika  shule mbalimbali za sekondari mkoani Mwanza, mkurugenzi wa Stoppers Entertainment ambao ndio waandaji wa shindano hilo, Bwana Mukhsin Mambo, amesema jumla ya shule 32 kutoka mkoani Mwanza, zitashiriki katika shindano hilo ambalo ni la kwanza kufanyika mkoani humo na Tanzania kwa ujumla.
Mambo, amesema shindano hilo pia litaonyeshwa kwenye moja ya runinga hapa nchini kuwapa fursa watazamaji kushuhudia vipaji vya wanafunzi katika kujieleza mbele ya jamii.
Amesema nia na madhumuni ya shjindano hilo, mbali na kuondoka na kitita cha zawadi kwa washindi lakini pia ni njia mojawapo ya kuinua kiwango cha elimu hapa nchini kwa wanafunzi kupata nafasi ya kujieleza mbele za watu, kufanya utafiti kutokana na mada itakayowekwa mezani, kuweka mahusiano mema dhidi ya wanafunzi na kujenga kizazi kipya katika nyanja ya elimu kupitia mfumo wa mijadala.
Miongoni mwa shule zitakazoshiriki shindano hilo ni pamojana Nsumba sekondari, Nganza Sekondari, Butimba sekondari, St. Joseph Girls Sekondari, Buswelu Sekondari, New Hellen Sekondari, Hill crest Sekondari, Bismark Sekondari

No comments: