22.11.13

Thursday, August 22, 2013

(News) TUNDA MAN akanusha habari zilizotolewa kwenye blog moja hapa Bongo.

Msanii anayeiwakilisha kundi la Tip Top anajulikana kwa jina la Tunda Man amezungumza na DJCHOKAblog na kusema kuna habari zimeandikwa kwenye blog moja hapa bongo inayojulikana kwa jina la MPEKUZI kuwa habari hizo si za kweli. Namnukuu akisema
"Choka hizi habari zingine si za kweli kabisa ni kuchafuliana jina tu hapa nchini, nadhani imefika wakati wa kuandika vitu na kufuatilia pande zote mbili sio kusikiliza pande moja na kutoa taarifa bila kusikiliza kwa yule unayetaka kumwandika. Mimi nalipwa sh ngapi kwenye show halafu nije kukimbia deni la laki 8 jamani, halafu isitoshe kama kweli ninamashtaka kwanini niwakimbie police?"

Ingia hapa kusoma mwenyewe jinsi ilivvyokuwa chanzo hicho cha habari kutoka kwenye blog ya MPEKUZI

No comments: