22.11.13

Friday, August 23, 2013

(News) Vodacom yazidi kusogeza zaidi huduma kwa wateja

 Ofisa Mkuu  wa Idara ya Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Hassan Saleh, akiteta jambo na mmliki wa duka la Vodacom, Ricky Renson,  lililoko Mzambarauni ,Gongo la Mboto, Jijini Dar es Salaam, Baada ya uzinduzi wa Duka hilo ambalo litatoa huduma kwa wakazi wa eneo hilo na maeneo ya jirani. Katikati ni Mke wa Mmiliki wa duka hilo Bi. Beatrice Renson.

 Ofisa Mkuu  wa Idara ya Mauzo na Usambazaji wa Vodacom, Hassan Saleh, akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani, wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Vodacom lililoko Mzambarauni , Gongo la Mboto, jijini Dar es Salaam, Duka hilo litatoa huduma kwa wakazi wa eneo hilo na maeneo ya jirani.

 Mmiliki wa duka jipya la Vodacom lililopo Mzambarauni , Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, Ricky Renson, akizungumza na waandishi wa habari, hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa duka hilo. Duka hilo litatoa huduma kwa wakazi wa eneo hilo na maeneo ya jirani. Katika ni Mke wa mmiliki wa duka hilo, Beatrice Renson na Mkuu wa kitengo cha Mauzo wa Vodacom Tanzania, Upendo Richard.

 Ofisa mkuu  wa Idara ya Mauzo na usambazaji wa Vodacom Tanzania, Hassan Saleh (wa kwanza kushoto) pamoja na Mkuu wa kitengo cha Mauzo wa kampuni hiyo  Upendo Richard na Mmiliki wa duka jipya la Vodacom lililoko Mzambarauni , Gongo la Mboto  jijini Dar es Salaam, Bi. Beatrice Renson  , wakifurahia mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa duka hilo.

 Ofisa mkuu  wa Idara ya Mauzo na usambazaji wa Vodacom Tanzania, Hassan Saleh, akimkabidhi funguo Mmiliki wa duka jipya la Vodacom lililopo Mzambarauni, Gongo la mboto, Ricky Renson, mara baada ya uzinduzi rasmi wa duka hilo linalofikisha idadi ya maduka 67 yanayotoa huduma kwa wateja  nchini. Katika ni Mkuu wa kitengo cha Mauzo wa kampuni hiyo  Upendo Richard na Mke wa Mmiliki wa duka hilo Bi. Beatrice Renson.

 Mmiliki wa duka jipya la Vodacom liliko Mzambarauni , Gongo la mboto jijini Dar es Salaam Bi. Beatrice Renson akifungua mlango kuashiria kuanza kwa huduma katika duka hilo mara baada ya uzinduzi huo. Katika ni Ofisa mkuu  wa Idara ya Mauzo na usambazaji wa Vodacom Tanzania, Hassan Saleh, na Mkuu wa kitengo cha Mauzo wa kampuni hiyo  Upendo Richard.

  Mfanyakazi wa duka jipya la Vodacom lililoko Mzambarauni , Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, John Kimwaga (Wa kwanza kushoto), akimuunganishia intaneti mmoja wa wateja aliyefika kupata huduma katika duka hilo, Bw. Venant Mlokozi. Anayeshuhudia ni  Ofisa mkuu  wa Idara ya Mauzo na usambazaji wa Vodacom Tanzania, Bw. Hassan Saleh.

Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania, Elihuruma Ngowi na Upendo Happiness Macha wakifungua Shampeni kuashiria uzinduzi wa duka jipya la Vodacom lililoko Mzambarauni, Gongo la mboto  jijini Dar es Salaam.

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Vodacom yasogeza zaidi huduma kwa wateja
Agosti 23, 2013 …KATIKA kukidhi haja ya utoaji wa huduma kwa wateja nchini, Kampuni ya Vodacom Tanzania imeendelea kupanua wigo wa huduma zake kwa kufungua duka jipya (Vodashop) katika eneo la Gongo lamboto jijini Dar es Salaam.
Ufunguzi wa duka hilo ni katika harakati za kuendelea kusogeza huduma za mawasiliano karibu na wateja na kufanya mauzo ya bidhaa mbalimbali za mtandao huo kuwa karibu zaidi ikiwemo huduma za kutuma na kupokea fedha (M-PESA), Intaneti, sambamba na vifurushi mbalimbali.
Akizungumzia wakati wa uzinduzi wa maduka hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Rene Meza, alisema Vodacom ni kampuni pekee ambayo imeendelea kuongoza kwa kuwa na maduka mengi ya mauzo na huduma kwa wateja kwa kufikisha maduka 67 kwa jijini Dar es Salaam huku ikitarajia kufungua maduka mengine zaidi.
Aliongeza kuwa ili kufanikisha azma ya kukidhi mahitaji ya huduma kwa wateja wa kampuni hiyo --Vodacom Tanzania imeamua kuongeza idadi ya maduka yake jijini Dar es Salaam kufikia 24 kutokana na mahitaji makubwa zaidi.
“Ukuaji wa huduma kwa kampuni ya Vodacom umekuwa mkubwa sana, huduma kama ya M – Pesa sasa imepanuka kwa kasi ambapo kwa sasa kampuni yetu inatoa huduma kwa watanzania zaidi ya milioni 20. Hivyo, kufuatia mafanikio haya tunalazimika kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya uhakika kwa wateja wetu,” alisema Bw. Meza, na kuongeza kuwa, “Kuongoza katika sekta ya mawasilaino kuna changamoto zake,hivyo ni lazima tuhakikishe tunaendana na kasi ya ukuaji wa huduma zetu ili kuendana na ongezeko la watu wa aina mbalimbali.”
Aidha Bw. Meza alisema kuwa kufunguliwa kwa duka hilo hivi sasa si tu kunaboresha upatikanaji wa huduma bali ni fursa pekee ya kuendelea kupanua wigo wa ajira kwa watanzania.
“Ufunguzi wa duka hili unatoa fursa ya ajira kwa Watanzania. Halikadhalika ufunguzi huu umejumuisha  ajira kwa wafanyakazi zaidi ya 10 ambao watatoa huduma kwa wateja wetu hivyo ni hatua kubwa tumetengeneza ajira kwa wafanyakazi wapya. Hadi kufikia sasa, Vodacom imetoa ajira za moja kwa moja kwa wafanyakazi 500 na wengine zaidi ya 30,000 wenye ajira zisizo za moja kwa moja,” alisema.
 
Kufuatia uzinduzi wa duka hilo la huduma za mawasiliano ya simu maeneo ya Gongolamboto, Kampuni ya Vodacom iko mbioni kufungua maduka mengine katika maeneo ya Kimara, Kigogo, na Msimbazi hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Upanuzi huu wa wigo wa huduma za mawasiliano ya simu wa Kampuni ya Vodacom Tanzania unafuatia uwekezaji kwenye mfumo wa mawasiliano wa 3G na 4G mfumo ambao unaotumia teknolojia mpya ya mawasiliano kazi iliyofanywa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania.
MWISHO

No comments: