Kundi la kwanza la wasanii
watakaotumbuiza katika tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2013 limewasili
mkoani Kigoma kwa ajili ya onyesho hilo. Wasanii hao 8 ni kati ya 12
watakaopanda katika jukwaa moja uwanja wa Lake Tanganyika siku ya
Jumamosi. Kundi la pili la wasanii ambao ni Profesa Jay, Diamond, Lady
Jaydee na Barnaba wanatarajiwa kuwasili siku ya Jumamosi asubuhi.
Baada ya kupata mlo wa mchana
ulioandaliwa na mwenyeji wao ambaye ni Doctor Gerrard Mipango wasanii
hao walipata nafasi ya kutembelea makumbusho ya Doctor Livingistone
yaliyoko Ujiji na kujionea historia mbalimbali ya mzungu huyo
anayetambuliwa kama mvumbuzi wa Ziwa Tanganyika na pia kuona maeneo
biashara ya utumwa ilipokuwa ikifanyika na kujifunza kuhusu asili ya
wenyeji wa Mkoa wa Kigoma.
No comments:
Post a Comment