Bi. Prisca George (kulia) mkazi kutoka Tegeta, Dar es Salaam, anahesabu kitita
cha mpoko alichopokea kupitia mradi wa MWEI unaoendeshwa na kampuni ya Vodacom Tanzania.
Bi. Prisca ni mmoja wa wanawake wajasiliamali 150 waliopokea mikopo isiyo na
riba ya jumla ya millioni kumi kupitia mradi wa MWEI eneo ya Tegeta ili
kuendesha biashara zao. Kulia ni Bi. Grace Lyon, Meneja wa Mradi wa MWEI na
katikati ni Bi. Zawadi Bakari, wakala wa M-Pesa.
Bi Zaituni Abdalla (kushoto) mkazi kutoka Tegeta, Dar es Salaam, anahesabu
kitita cha mpoko alichopokea kupitia mradi wa MWEI unaoendeshwa na kampuni ya Vodacom
Tanzania. Bi. Zaituni ni mmoja wa wanawake wajasiliamali 150 waliopokea mikopo
isiyo na riba ya jumla ya millioni kumi kupitia mradi wa MWEI eneo ya Tegeta
ili kuendesha biashara zao. Anayeshuhudia ni Bi Rukia Mtingwa, Meneja
Mawasiliano Vodacom Tanzania.
Bw.
Martin Kiswaga (kulia) ofisa kutoka kampuni ya Vodacom Tanzania, akielezea
kikundi cha wanawake wajasiliamali kutoka Tegeta, Dar es Salaam, jinsi chaja ya
ReadySet inavyofanya kazi. Chaja hio ilizinduliwa na kampuni ya Vodacom na
inatumia nishati ya jua kuchaji simu kumi wakati mmoja. Wanawake hao pia
walipata mikopo isiyo na riba kupitia mradi wa MWEI ya ujumla ya million kumi.
No comments:
Post a Comment