22.11.13

Monday, September 23, 2013

(News) Kukosekana kwa huduma ya M-Pesa nchini tarehe 21 Septemba, 2013

Tunapenda kuwaomba radhi wapendwa wateja wetu, washirika wetu na benki zote pamoja na wananchi wote kwa ujumla kwa kutoweza kutumia huduma yetu ya M-pesa kutokana na kazi ya kuboreshwa kwa mtandao wa huduma ya M-Pesa. Kazi hiyo ilipangwa kufanyika kuanzia saa 6 usiku na kumalizika saa kumi alfajiri siku ya tarehe 21 Septemba, 2013.
Kazi ya uboreshaji wa mtandao huo ilikwenda vizuri, lakini mabadiliko hayo yalipelekea kutokea kwa matatizo kadhaa ya kiufundi ambayo yalidumu kwa muda wa saa 8, hali ambayo iliyotulazimu kusitisha baadhi ya huduma za mtandao wa M-Pesa.
Mafundi wetu walifanya kazi kwa bidii na umakini mkubwa na hatimaye waliweza kutambua na kutatua chanzo cha matatizo hayo yaliyosababisha kusimama kwa baadhi ya huduma za M-Pesa nchini. Mtandao wa huduma za M-Pesa ulioboreshwa ulitengemaaa na kurudi katika hali yake ya kawaida siku hiyo hiyo saa 11:30 jioni.
Kwa mara nyingine tena ninaomba niwatake radhi wateja wetu na washirika wetu wote pamoja na jamii kwa ujumla kwa usumbufu walioupata kutokana na kutopatikana kwa huduma za M-Pesa nchini. Aidha, ninawashukuru nyote kwa uaminifu wenu wa kuendelea kuziamini na kuzitumia huduma za M-Pesa kukidhi mahitaji yenu ya kila siku.
Rene Meza
Mkurugenzi Mtendaji
Vodacom Tanzania Limited

No comments: