22.11.13

Monday, September 02, 2013

(News) Mulugo asisitiza ushiriki wa kila mtanzania katika kuendeleza elimu

 Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi Phillip Mulugo akifurahia jambo na Meneja Masoko wa Mikono Business Consult Bi. Nestoria Simon (kushoto)na Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule mara baada ya kuelimishwa kuhusu na matumizi bora  ya pedi kwa wanafunzi wakike waliopo mashuleni,alipofika katika uzinduzi wa maonesho ya Vodacom Elimu Expo yaliyofanyika katika viwanja vya posta kijitonyama jijini Dar es salaam.

 Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi Phillip Mulugo,akifafanuliwa jambo na  Meneja masoko wa Vodacom M-PESA Bw.Nixon Bonaventure,alipotembelea banda la kampuni hiyo mara baada ya kuzindua rasmi maonesho ya Vodacom Elimu Expo yaliyofanyika  kwa siku tatu katika viwanja vya posta kijitonyama jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi Phillip Mulugo,akifafanuliwa jambo na  Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano Bw.Kelvin Twissa kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Vodacom hususani  M-PESA kwenye sekta ya Elimu nchini,alipofika katika viwanja vya posta kijitonyama jijini Dar es salaam,kuzindua  maonesho ya Vodacom Elimu Expo yaliyofanyika  kwa siku tatu. 


Mulugo asisitiza ushiriki wa kila mtanzania katika kuendeleza elimu
 
Dar es Salaam, Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo, amewaasa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kutumia teknolojia ya elimu masafa na mitandao kwa kupata taarifa za uhakika za kitaluma na kimaendeleo.
 
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Vodacom Elimu Expo 2013 juzi, jijini Dar es Dalaam, Waziri Mulugo alisisitiza kuwa ushiriki wa wandau wote kuendeleza sekta ya elimu inafungua fursa ya kupata na kutoa elimu bora kwa kila mtanzania.
 
Maonesho ya Vodacom Elimu Expo 2013 ni ya kwanza Tanzania yaliodhaminiwa na kampuni ya simu ya Vodacom kupitia huduma yake ya M-Pesa inayowezesha malipo ya karo ya shule kwa urahisi zaidi.
 
Waziri Mulungo alisema: ““Hii ni fursa kubwa sana kwa wote wanaoshiriki maonesho haya ususani wanafunzi, walimu na wazazi. Yanatoa nafasi kwa kila mdau wa elimu kuchangia maendeleo ya elimu nchini. Na hasa ukizingatia kukuwa kwa matumizi ya mtanda na simu za mkononi katika kila kaya, ni fursa kubwa katika kubadilishana mawazo ya kujenga Tanzania yenye elimu bora na shindani katika Nyanja za kimataifa.”
 
Alidokeza kuwa Serikali kupitia wizara ya elimu, ipo katika hatua za mwisho za kutengeneza mkongo wa taifa utakao unganisha upatikanaji wa mtandao nchi nzima kapitia program ijulikanayo kama ‘Tanzania Beyond Tomorrow’ kwa kushirikiana na makampuni ya mawasiliano katika kuboresha elimu masafa yaani”e-learning”.
Naipongeza kampuni ya Vodacom kwa kuwa kampuni ya kwanza nchini kushirikiana na Serikali kutekeleza mpango huu katika kuhakikisha kuwa sekta ya elimu inaendelea na kuwa bora zaidi. Sasa ni rahisi kwetu wazazi kutumia njia bora, tena ya uhakika naya kuhaminika ya M-Pesa kulipia watoto wetu karo ya shule,” alisema Mulugo.
 
Naye Robert Mihalo, ambaye ni mwanafuzi wa shule ya green acres ya jijini alipongeza wadhamini na waandaji wa maonyesho hayo akisema: “Nimeweza kubandilishana mawazo na wanafunzi wa shule zingine. Zaidi ya yote, nimepata mbinu mpya kwa kupanua wigo wa ushiriki wa wanafunzi katika kuleta elimu bora Tanzania.”
 
Maonesho haya ni muhimu sana kwani yanawaelimisha wananchi kuhusiana na Vodacom Elimu Expo 2013 ambayo itaaanza kutoa taarifa muhimu zinazohusu shule mbalimbali ikiwa ni pamoja na gharama za ada na michango mingine katika shule husika.Aidha itaendelea kutoa taarifa zinazohusu vyuo na taasisi za elimu ya juu ikiwa pamoja na fani zitolewazo katika vyuo husika pamoja na gharama zake kupitia simu za viganjani,tovuti na blogs za elimu.
Nae Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa,ambao ni wadhamini wakuu wa maonesho hayo  alionyesha matumaini yake kwa maonesho hayo na kusema kampuni yake inaelewa umuhimu wa elimu kwa kila mtoto kwa hiyo wanajisikia fahari kudhamini maonesho hayo kwani yanalenga kuboresha elimu ya Tanzania.
Wadhamini wengine wa Maonesho hayo ni :- Clouds FM, DTV, Entertainment Masters, Maxmalipo, Times FM, Primebiz Solutions Ltd na bima ya taifa ya afya, NSSF, Azania Bank, FNB, Primebiz, NHIF, IPS, NMB, Global publishers, DSTV, Clouds FM.
Mwisho.

No comments: