22.11.13

Thursday, September 19, 2013

(News) SAM WA UKWELI: PAPAA MISIFA ALINIANGUSHA KIMUZIKA ILA K WA SASA NIMERUDI TENA

Papaa misifa kiukweli alicho nifanyia sio kizuri mpaka nujuta kuwa chini yake naamini kama ningeendelea mwenyewe ningekua sehemu nzuri atakama sio sana lakini nisingekua apa hasa kua kimywa kimuziki.Niliingia kwenye imaya ya Papa baada ya kuachia ngoma yangu ya SINA RAHA na HATA KWATU WAPO ambazo zilifafanya vizuri wakati najiongoza mwenyewe na baadhi ya jamaa zangu walio kuwa wananipa sapoti za apa na pale yeye ndo akanijua toka apo niliingia nae mkataba wa miaka miwili (2) ambao tulikubaliana vizuri kabisa na masharti ya kufanya kazi kila baada ya muda Fulani nifanye ngoma kadhaa.

Kibaya alicho kifanya yeye akasahau majukumu yake na kuzubaa na kazi ambazo mimi nilitoka nazo kwangu na zikawa zinafanya vizuri wakati uwo katika radio na Tv tofauti za apa na nje ya ncnchi yetu bila kusahau kwenye Kampuni pia za simu za mikononi kama ring tone . Uko kote zikawa zinatoka pesa ambazo nilizifanyia mimi kazi katika ngoma zile mbili nilizofanya wakati niko mwenyewe ,Hata show ilikua nikipata tunagawana nusu kwa nusu wakati yeye hakutoa chochote kuhusiana na nyimbo izo nilienda pale kwa kufanya kazi ambazo tulikubaliana lakini ule mkataba ukanigeukia mimi tena na kazi zangu za mwanzo kwa sababu aliona kuna maslahi binafsi. Mimi nilikubaliana na ali hiyo nikataka tuanze kufanya kazi ambazo zitaniweka sehemu nyingine apo sasa ndipo ulipoanza utata akawa apendi kutoa pesa ila anataka kupokea pesa.
 
Ngoja niwape uthibitisho kidogo kuna wimbo nilirekodi chini yake kwa shida sana sasa ikawa zamu ya kuifanyia video na tulipanga tuifanye kwa Adam Juma basi nilizungushwa mpaka nilikata tama,jibu lake
“Adam Juma anaratiba ndefu sana we subuli tu tutafanya akitulia”Sasa kuna siku ikafika kama ilivyo mungu amtupi mja wake nikawa naenda kumsaidia rafiki yangu TIMBULO kufanya video yake WALEO WA KESHO kwa uyouyo Adam Juma ndo nikamuuliza kuhusu mchongo mzima na kuwa kapewa pesa nusu ya kazi yangu alikataa na kusema “Uongozi wako unatabia ya ubabaishaji na ata hii video nafanya sijui kama nitamaliziwa pesa ilio baki mwana” Basi toka apo nikafahamu kuwa nilipo ingia sipo nikaomba nivunje mkataba nikaambiwa nikivunja tu nahitajika nilipe pesa za kitanzania zisizo pungua miliono 100 nikaogopa ndo nikapata akili ya kukaa bila kufanya kazi yoyote tuangaliane mpaka mkataba wake uishe nikawa naishi kwa pesa za ring tone napo akawa anaingilia mapa uko ata ivi namdai pesa zangu za mwezi huu wa tisa(9) na mkataba wake ndo umeisha tayari na ndio maana nimefanya kazi yangu mpya nimeweka sumu za mjini Rich mavoko na Zed Anto inafahamika kama AMESHA OLEWA ambayo kwa sasa iko kwenye mikono yenu naomba msiitupe MUNGU AWABARIKI AMEN

No comments: