22.11.13

Tuesday, September 17, 2013

(News) Severina Lwinga Atwaa taji la Miss Tanzania Personality 2013

Mrembo Severina Lwinga juzi alifanikiwa kuwa mrembo wa tano kuingia nusu fainali ya shindano la Redd's Miss Tanzania 2013 baada ya kutwaa taji la Miss Personality 2013. Mshindi wa taji hilo anapatikana kwa kupigigiwa kura na warembo wenzake.

Severina ameungana na Miss Tanzania Photogenic 2013, Happiness Watimanywa, Miss Tanzania Talent 2013, Prisca Clement, Miss Tanzania Top Model 2013, Narietha Boniface na Miss Tanzania Sports Woman, Clara Bayo kuingia katika nusu fainali ya Miss Tanzania ambayo itafanyika Jumamosi hii ukumbi wa Mlimani City. Shindano hilo lilifanyika Mgahawa wa AK'S ulipo mtaa wa Samora.
 

No comments: