22.11.13

Tuesday, October 08, 2013

Hii ndio Artwork ya wimbo mpya wa JAY MOE unaokuja.

Mteule Juma Mchopanga a.k.a Jay Moe, More Techniques amewakutanisha wakali wa Bongo Fleva Mr. Blue, Cpwaa na AY kwa kuwashirikisha kwenye wimbo wake unaotarajiwa kutoka hivi karibuni na umepikwa na producer P-Funk Majani wa Bongo Records.
 Wimbo huo umepewa jina la CBM ikimaanisha ‘Check Bob Maarifa’. Mmoja kati ya washiriki katika Project hiyo Mr.Blue Byser ameongea na tovuti ya Timesfm kuhusu project hiyo ambapo amesema project hiyo ni kubwa na iko chini usimamizi mkubwa.
“Mi naweza kusema Project ni nzuri, na ni project kubwa, kama unavyoona imefanywa na watu hawa wakubwa. Pia ni Project ambayo ina nguvu sana, kwa hiyo usimamizi wake ni mkubwa chini ya P-Funk Majani mwenyewe au sio..kwa hiyo fans wa Jay Moe wategemee kitu kikubwa sana kutoka kwa Jay Moe, na fans wa CP hali kadhalika fans wa AY na Mr. Blue.” Amesema Byser.
P Funk Majani ametweet kuhusu ngoma hiyo ya Jay Moe ambae yuko nje ya nchi hivi sasa, BMS inaweza kusikika kwenye vituo vya radio hivi punde kwa mujibu wa Majani. So endelea kusikiliza Timesfm 100.5 au kama uko nje ya Dar es Salaam unaweza kusikiliza online kupitia tovuti hii.  
“CBM Coming Soon to a Radio Near You!” Ametweet P-Funk Majani.

5 comments:

sharo gangstar said...

Hopefull itakua poa xana

Anonymous said...

mafundi hao lazima mzigo uwe pouwaaaaaa!!

ISA MBWANA said...

MAjani kwenye kick,masnare akosei much respect m@ bro...ther/pale mo tech,huku byser,hapo cp yule pale mzee wa abroad kutoka mzee wa comercial mtaani kuchungu kwa wabana puuu....kubayaaa

ISA MBWANA said...

MAjan noma,mo,blue,cp&ay bonge la project

ISA MBWANA said...

MAjani kwenye kick,masnare akosei much respect m@ bro...ther/pale mo tech,huku byser,hapo cp yule pale mzee wa abroad kutoka mzee wa comercial mtaani kuchungu kwa wabana puuu....kubayaaa