22.11.13

Saturday, October 12, 2013

(News) MSTAHIKI MEYA WA ILALA AKABIDHIWA KATONI 50 ZA MAJI NA FULANA 1,000 TOKA VODACOM TANZANIA

 Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania,Bw.Salum Mwalim akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kukabidhi katoni hamsini za maji na fulana 1,000 kutoka Vodacom kusaidia matembezi ya hisani yanayofanyika kesho Jumamosi 12 Oktoba, 2013 jijini Dar es salaam kuleta hamasa kwa wananchi kuchangia kampeni ya kumaliza uhaba wa madawati katika Manispaa ya Ilala. Kushoto ni Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Jerry Silaa aliyendaa matembezi hayo.

 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kupokea katoni hamsini za maji na fulana 1,000 kutoka Vodacom kusaidia matembezi ya hisani yanayofanyika kesho (Jumamosi 12 Oktoba, 2013) jijini Dar es salaam kuibua hamasa kwa wananchi kuchangia kampeni ya kumaliza uhaba wa madawati katika Manispaa ya Ilala. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania,Bw. Salum Mwalim

 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (wa pili kushoto) na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim wakionesha kwa waandishi wa habari fulana zilizotolewa na Vodacom kusaidia matembezi ya  hisani yanayofanyika kesho Jumamosi 12 Oktoba, 2013 kuibua hamasa kwa wananchi kuchangia kampeni ya kumaliza uhaba wa madawati katika Manispaa ya Ilala. Vodacom imetoa fulana 1,000 na maji katoni 50. Wengine pichani ni  Zainabu Katimba na Halima Bulembo wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam waliojitolea kusaidia usimamizi wa matembezi hayo.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa(wa pili kuhsoto) akipokea kutoka kwa Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim sehemu ya fulana 1,000 zilizotolewa na Vodacom kusaidia matembezi ya hisani ya kuhamasisha jamii kuchangia kampeni ya kumaliza uhaba wa madawati katika Manispaa ya Ilala.  Wengine pichani ni  Zainabu Katimba (kushoto) na Halima Bulembo wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam waliojitolea kusaidia usimamizi wa matembezi hayo.

No comments: