22.11.13

Thursday, October 24, 2013

(News) 35 watimka na Boda Boda za Vodacom

 Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu(katikati)akimuonesha namba ya simu Msimamizi wa bodi ya  Michezo ya kubahatisha nchini,Bw.Abdallah Hemed,aihakiki kabla ya kumpigia mmoja kati ya washindi(5)aliejishindia Pikipiki katika promosheni ya”Timka na Bodaboda”inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,Jumla ya washindi(5)wamejishindia Pikipiki na wengine(2)wamejinyakulia shilingi Milioni moja moja.Ili kujiunga na promosheni hii TUMA NENO PROMO kwenda 15544,kushoto ni Afisa wa huduma za ziada wa kampuni hiyo Rashid Maggid.

 Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu,akisisitiza jambo kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani)kuhusiana na umuhimu wa watanzania na wateja wa Vodacom kushiriki katika Promosheni ya ”Timka na Bodaboda”Jumla ya washindi(5)wamejishindia Pikipiki na wengine(2)wamejinyakulia shilingi Milioni moja moja.Ili kujiunga na promosheni hii TUMA NENO PROMO kwenda 15544,kulia ni Msimamizi wa bodi ya  Michezo ya kubahatisha nchini,Bw.Abdallah Hemed.

 Mshindi wa Pikipiki katika Promosheni ya”Timka na Boda Boda”Bw.Dominick Leonard,mkazi wa jijini Dare s Salaam akionesha funguo wake wa pikipiki mara baada ya kukabidhiwa na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu(kulia) Jumla ya washindi(5)wamejishindia Pikipiki na wengine(2)wamejinyakulia shilingi Milioni moja moja katika droo ya leo.Ili kujiunga na promosheni hii TUMA NENO PROMO kwenda 15544,anayeshuhudia kushoto ni Afisa huduma za ziada wa kampuni hiyo Rashid Maggid.

 Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu,akimvisha kofia ngumu(Helmet) Mshindi wa Pikipiki katika Promosheni ya”Timka na Boda Boda”Bw.Dominick Leonard,mkazi wa jijini Dare s Salaam.Jumla ya washindi(5)wamejishindia Pikipiki na wengine(2)wamejinyakulia shilingi Milioni moja moja katika droo ya leo.Ili kujiunga na promosheni hii TUMA NENO PROMO kwenda 15544,kushoto anayeshuhudia ni Afisa huduma za ziada wa kampuni hiyo Rashid Maggid.

 Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu,(kulia mwenye shati jekundu)akiwatambulisha baadhi ya washindi(6)wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojishindia pikipiki katika Promosheni ya”Timka na Boda Boda”inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,Katika droo ya leo washindi(5)wamejishindia Pikipiki na wengine(2)wamejinyakulia shilingi Milioni moja moja.Ili kujiunga na promosheni hii TUMA NENO PROMO kwenda 15544

 Baadhi ya washindi wa pikipiki ambao ni wakazi  wa jiji la  Dare s Salaam, wakiziendesha pikipiki zao kwenye makao makuu ya kampuni ya Vodacom yaliyopo Mlimani city walizojishindia katika Promosheni ya ”Timka na Boda Boda” inayoendeshwa na kampuni hiyo mara  baada ya kukabidhiwa na Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Bw.Matina Nkurlu(hayupo pichani)

 Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu,akimvisha kofia ngumu(Helmet) Mshindi wa Pikipiki katika Promosheni ya”Timka na Boda Boda”Bi.Hellen Egbertbaada ya kuwakabidhi washindi (5)pikipiki zao mara baada ya kuibuka washindi kakatika promosheni hiyo . Jumla ya washindi(5)wamejishindia Pikipiki na wengine(2)wamejinyakulia shilingi Milioni moja moja katika droo ya leo.Ili kujiunga na promosheni hii TUMA NENO PROMO kwenda 15544. 

Mshindi wa Pikipiki katika Promosheni ya”Timka na Boda Boda”Bw.Dominick Leonard,mkazi wa jijini Dare s Salaam akiwasha pikipiki yake aliyejishindia katika promosheni hiyo mara baada ya  kukabidhiwa na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu(kulia) Jumla ya washindi(5)wamejishindia Pikipiki na wengine(2)wamejinyakulia shilingi Milioni moja moja katika droo ya leo.Ili kujiunga na promosheni hii TUMA NENO PROMO kwenda 15544,anayeshuhudia kushoto ni Afisa huduma za ziada wa kampuni hiyo Rashid Maggid.

35 watimka na Boda Boda za Vodacom
Dar es Salaam, 24 Septemba, 2013 … Hakika maisha ya maelfu ya Watanzania yanaendelea kuboreshwa siku hadi siku, haya yote ni kupitiaPromosheni ya Timka na Boda Boda”inayoendeshwa na kampuni inayoongoza nchini ya Vodacom Tanzania. Jumla ya Watanzania 35 wamejishindia usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu, amesema siku zote Vodacom imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inaboresha maisha ya wateja wake ambao mchango wao umeifanya kampuni hiyo kuendelea kuwa namba moja kupitia Promosheni mbalimbali wanazoziendesha.
“Lengo letu sisi kama Vodacom ni kuhakikisha tunaendelea kuimarisha maisha ya wateja wetu ambao wamekuwa wakituunga mkono siku zote, Tunaamini kuwa kwa kuboresha maisha ya wateja wetu kutoka katika faida tunayoipata ili kuwawezesha wao kuendelea pia kutuunga mkono siku hadi siku na kwa nguvu zaidi,” alisema Nkurlu na kuongeza
“Tumetambua tatizo kubwa la ugumu wa maisha unaoikabili jamii ya Watanzania hususani Vijana, hivyo kupitia zawadi hizi za Pikipiki zenye gharama ya zaidi ya Bilioni 1.6 wananchi wataweza kujiajiri huku wakipunguza gharama za usafiri, aliongeza.
Nkurlu amesema Watanzania wengi wamekuwa na ndoto za kuendesha maisha yao kupitia shughuli za ujasiriamali ambapo kwa kutambua hilo wametoa fursa hiyo ili kutimiza matajario yao yenye lengo la kujikwamua kwenye umaskini.
Hadi sasa takwimu za washindi zinaonesha kwamba kati ya Bodaboda 30 zilizoshindaniwa 8 kati ya hizo zimeenda Mkoani Arusha ambapo karibia washindi wake wote wajasiriamali jambo ambalo limeleta mrejesho wa promosheni hii.
Kwa upande wake mmoja wa washindi wa Promosheni hiyo Ramadhani Saidi Shabani (40) akizungumza kwa njia ya simu kutoka Arusha alisema anaishukuru Kampuni ya Vodacom kwa kumpatia fursa ya kuweza kujishindia usafiri huo.
“Najisikia Fahari kuwa mteja wa Vodacom, wameniboreshea maisha yangu kwa kunipa nafasi ya kujishindia Boda Boda sasa nina uhakika wa kuboresha maisha yangu huku nikipunguza gharama za fedha nilizokuwa nikizitumia kwa kusafiri kutoka eneo moja hadi nyingine,” Alisema Shabani.
Katika Promosheni hii ya Timka na Boda Boda kampuni Vodacom imetenga jumla ya bodaboda 430 kwa kipindi cha siku 100. Ili kupata nafasi ya kujishindia bodaboda hizo, na shilingi milioni moja kila siku mteja wa Vodacom atatakiwa kutuma ujumbe wenye neno PROMO kwenda 15544.
Mwisho...

No comments: