Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya Msingi Sinza Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es
Salaam,wakifundishwa
jinsi ya kuandika mwandiko mzuri na Ofisa kitengo cha mikopo wa Benki
ya KCB Tanzania, Bw. Innocent Mlimuka walipofika shuleni hapo kutoa
msaada wa madawati 100 shuleni hapo.
Mwalimu
Venancia Venant (watatu toka kushoto waliokaa) wa shule ya Msingi
Makumbusho Wilaya ya Kinondoni
jijini Dar es Salaam,akisikiliza jambo toka kwa Ofisa wa kitengo cha
mikopo wa Benki ya KCB Tanzania, Bw. Innocent Mlimuka mara baada ya
kukabidhiwa msaada wa madawati 100 kutoka benki hiyo kwaajili ya
matumizi ya wanafunzi wa shuleni hiyo.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya Msingi Sinza Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es
Salaam, wakimsikiliza
Meneja Uhusiano wa Umma wa benki ya KCB Tanzania, Bi. Hellen Siria
alivyokuwa akiwaelezea umuhimu wa Elimu na kutunza madawati 100
waliyopewa msaada na benki hiyo kwa manufaa ya wanafunzi wengine.
Afisa
Elimu kata ya Msasani,Bw.Kebero Maulid,akipanda mti katika shule ya
Msingi Mbuyuni iliyopo
Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam,Jumla ya miti Elfu mbili na
Madawati 100 yalitolewa msaada na Benki ya KCB Tanzania kwa ajili ya
shule za msingi 6 na sekondari moja ya oysterbay zote za Wilaya ya
Kinondoni jijini Dar es Salaam,anaeshuhudia kulia
ni Mwfanyakazi wa benki hiyo,Bw.Tito Mbise.
No comments:
Post a Comment