22.11.13

Wednesday, October 16, 2013

(News) DJ CHOKA KUPATA MTOTO MWINGINE MPYA TAREHE HII.

Habari wadau wa DJCHOKAblog
Tarehe 22/11/2013 natarajia kufungua website mpya ambayo itakuwa inaitwa DJ CHOKA MUSIC, website hii itakuwa kama ilivyo DJCHOKAblog vile vile sema itakuwa katika muonekano wa kiwebsite pamoja na jina jipya tu ndicho kilichobadilika.

Dhumuni la kuwa na website ni kutokana na maoni mengi ya wadau walikuwa wakiomba kweli kweli tuhamie kwenye website mbali na kununua domain ila hadi theme nzima ya site ibadilike. Maoni yenu nimeyasikiliza na imeyafanyia kazi na kitu kipo jikoni tayari kwa kupakuliwa siku hiyo. 

Najua mtajiuliza kwanini imekuwa siku ya tarehe hiyo, nimeweka tarehe hiyo kwasababu siku hiyo itakuwa kumbukumbu ya kuzaliwa mwanangu Harrison na atakuwa anatimiza mwaka mmoja so nikaona sio mbaya siku hiyo muhimu na mimi nikizindua site yangu ili iwe kumbukumbu tosha kwangu na kwa mwanangu kwasababu blog hii ndio inanyomfanya yeye apate malezi bora na mazuri siku zote nazoangaika kutafuta matukio usiku ili yeye tu aishi vizuri.

Natumaini mtanipokea vizuri katika website hiyo ya DJCHOKA MUSIC na hamtoniangusha maana bila nyie hakuna DJ Choka naomba tumpokee mtoto huyu mpya. Nawatakia sikukuu njema ya Eid pamoja na kazi njema mrudiapo makazini.

Nawapenda sana

DJ CHOKA