Member wa B Hitz Music Group Dj Choka ambae anafanya project
za Hip Hop kwa kuwaunganisha wasanii wenye uwezo mkubwa wa kurap, na
kuwaweka kwenye wimbo mmoja, amesema anampango wa kuwapa deal hiyo pia
wasichana watatu wanaojua kurap vizuri lakini hawajatoka.
“Nafikiria tena kufanya ngoma na wasichana wanaorap lakini wakali,
yaani nataka nikipata wawili lakini wawe wanarap ile yenyewe yani,
haijalishi Kiswahili au kiingereza. Unajua kwenye ngoma zangu mi naona
namuweka tu Vanessa Mdee, unajua Vanessa anaimba lakini akija kwenye
project yangu inabidi achane.” Amesema Dj Choka.
Kuhusu sifa na jinsi ya kuwapata wasichana hao, alifunguka,
“nafikiria kufanya Ki-search kidogo hivi lakini ntawaambia kwa kuwa bado
ni mapema, nataka kufanya search ndogo tu ili nipate wasichana kama
watatu hivi ambao watakuwa wanarap,ntafanya search siku si nyingi tu
halafu ntawapata hao, kwa hiyo wakae mkao wa kula .”
Dj Choka hivi sasa anapika project yake anayofanya na wasanii kadhaa
wenye umri mdogo na tayari Young Dee, M-Rap, Janjaro na Country Boy
wameshaweka vocal ndani ya studio za BHitz, lakini Dj amesema zipo
project nyingine zitakazotangulia kutoka kabla ya project hiyo.
Source: TIMES FM
No comments:
Post a Comment