Pichani Mwanamuziki Profesor Jay akiwa na mfano wa hundi
yenye Barcode ambazo amekabidhiwa leo, Jay anakuwa mwanamuziki wa Pili kuchukua
Barcode za Tanzania katika sekta ya muziki wa Bongo Fleva nchini.
Hayo yamesemwa leo na mwanamuziki Profesa Jay alipokuwa
akikabidhiwa Barcode za ajili ya CD yake mpya itakayojulikana kama The Best of
Professor Jay ambayo itakuwa na mchanganyiko wa nyimbo zake ambazo zime heat
tangu kuanza kwake. “nimeamua kutoka kivingine na kwa sasa nataka kufanya vitu
kimataifa kwa kusambaza kazi zangu kwenye mitandao ili niwafikie watu wengi
zaidi” alisema Jay.
Akiongea katika makabidhiano hayo Mwenyekiti wa Bodi ya GS1
Tanzania Bw. Elibariki Mmari alisema kuwa ni wakati muafaka kwa wanamuziki wa
Tanznia kuanza kuuza kwenye mitandao ya kijamii na masoko ya kwenye mtandao kama
wanavyofaidi fursa hizo wanamuziki wengine. Bwana Mmari alisema kuwa kwa kutumia
fursa hizo wanamuziki hao wanaweza kuuza kwenye mitandao ya kijamii kwa kupitia
makampuni makubwa duniani kama CD Baby ambalo lina mikataba na maduka yote
makubwa ya kwenye mtandao kama iTune, Facebook Music na mengine makubwa.
Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Bw. Elibariki Mmari (Mwenye
Koti la suti) akizungumza wakati wa halfa fupi ya kumkabidi Barcode mwanamuziki
wa Kizazi Kipya Profesa Jay katika makao makuu ya Ofisi hiyo TIRDO Msasani
jijini Dar Es Salaam, Kulia kwa Bw. Mmari ni Fatma Kange Saleh Afisa Mtendaji
Mkuu wa GS1 Tanzania na Nd. Pius Mikongoti Afisa Muandamizi toka GS1 Tanzania na
kushoto kwa Mwenyekiti ni Bw. Joseph Haule aka Profesa Jay.
Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Ndugu Mmari akimkabidi mfano
wa hundi yenye Barcode kwa ajili ya CD na nyimbo za mwanamuziki Profesa Jay huku
wajube wa Bodi ya GS1 Tanzania wakishuhudia.
Aidha Mwenyekiti Mmari alitanabaisha kuwa wanamuziki wa
Tanzania hawawezi kuingia kwenye chati kubwa kama za Billboard bila kuwa na
utambulisho wa ki electroniki wa Alama za Mistari yaani Barcode. Naye Afisa
muandamizi wa GS1 Tanzania Bw. Pius Mikongoti alisema kuwa ni vigumu kupata
takwimu sahihi za usambazaji za wanamuziki wa Tanzania kwani kazi zao haziko
kwenye mfumo rasmi, “ukiangalia mwanamuziki kama Lady Jay Dee mathalani ana
wafuasi wamefikia laki moja kwenye mtandao wake wa kijamii wa Facebook kama
atatangaza kuuza kazi zake kwenye mitandao hiyo ni wazi atawafiukia washabiki
wake kirahisi zaidi” Takwimu za Billboard zinachukuliwa kutokana na usambazaji
na mauzo ya kazi za mwanamuziki ki electroniki, ni vigumu kwa mwanamuziki kama
Diamond ambaye kwa sasa ana mashabiki lukuki na kazi zake kupigwa kila kona
kupata takwimu sahihi za usambazaji wake.
Aidha amewataka wadau wa muziki nchini kuacha kusambaza nyimbo
mpya za wanamuziki kwenye mitandao na kuwafanya watu waweze kuzipata bila
kuzitolea chochote (downloads), kwa kufanya hivyo tunawaumiza wanamuziki na
tunakuwa hatuwasaidiii aliongeza Bw. Mikongoti. GS1 Tanzania ndio watoaji pekee
wa huduma za BArcode kwa bidhaa zote za Tanzania, ikumbukwe kuwa ili uweze kuuza
kwenye Supermarket na masoko ya mitandaoni ni lazima uwe na alama hizi za
mistari yaani Barcode.
1 comment:
Hivi kuna msanii wa kizazi kipya wa kitanzania yeyote ambae kazi zake zinapatikana Spotify. Naumba msaada wadau
Post a Comment