22.11.13

Wednesday, October 16, 2013

(News) PROMOSHENI YA MKWANJA KWA WAKALA WA M-PESA YAANZA RASMI

 Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim, akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) Wakati wa kutangaza washindi wa Promosheni ya "Mkwanja kwa Wakala" ambayo inalenga kutambua na kuthamini  mchango wa Mawakala wa M pesa kwa kuwapa nafasi ya kujishindia fedha taslim kila wanapofanya miamala ya fedha kwa wateja huduma hiyo.Pamoja nao katika picha (Kushoto) ni Mkuu wa Kitengo cha Mauzo M Pesa, Franklin Bagalla na Mkuu wa kitengo cha Uendelezaji Biashara  M pesa, Isack Nchunda.

Mkuu wa Kitengo cha Mauzo M Pesa, Franklin Bagalla (Kushoto) na Mkuu wa kitengo cha Uendelezaji Biashara M Pesa, Isack Nchunda (Kulia)wakimshuhudia Meneja Uhusiano wa nje wa Kampuni hiyo Salum Mwalim, akiwaonesha waandishi wa habari (Hawapo Pichani) Namna ya kushiriki Mawakala wa M-PESA katika Promosheni ya "Mkwanja kwa Wakala" inayolenga kutambua na kuthamini mchango wa Mawakala wa M Pesa kwa kuwapatia nafasi ya kujishindia fedha taslim kwa kufanya miamala ya fedha kwa wateja wa mtandao huo.

No comments: