22.11.13

Tuesday, October 15, 2013

(News) SINA TIME NA MUZIKI TENA "NOORAH BABA STYLE"

Msanii wa Muda sasa kwenye Industry ya Bongo Fleva Noorah a.k.a BabaStyle amevunja ukimya kwa kuamua Kufunguka kile kilicho moyoni mwake kuhusu ukimya wake kwenye Game kwa sasa ambapo amefika mbali na kusema kuwa Mziki hauna faida kwake na kwa sasa anaufanya Mziki kama Starehe like mtu anavyotoka kwenda Bar kunywa beer huku akiwa sio Mlevi means siku akifeel ham tu.
Akizungumza na DJ HAAZU ndani ya Kipindi cha DUNDO ndani ya MJ RADIO Arusha Noorah ameelezea ukimya wake ambao yuko nao kwamba Kwa sasa mziki hautegemei tena kwamba utakuja kumpa faida kwani ameusotea kwa muda Mrefu sana bila Mafanikio na kusema kuwa Hana time nao tena bali ana mambo mengi ya kufanya yanayomuendeshea Maisha yake na sio muziki ila ataufanya tu kama sehemu ya Starehe.
Amejaribu kufafanua kuhusu wingi wa Wasanii kuwa wengi Nchini huku wenye Mafanikio wakiwa wachache ambao pia amewataja kama watu wa kusifiwa wana hela ila sio kiivyo ambapo wanasemwa wamefanikiwa kumbe ni maneno tu (Politics kwenye muziki).
POINT YA NOORAH INASEMA Maisha ni Malengo na kama kitu hakina faida nacho hakina maana kwako

MSIKILIZE NOORAH HAPA CHINI AKIONGEA NA HAAZU
click link hii hapa >>>  http://old.hulkshare.com/2cu41xc6wjy8

No comments: