22.11.13

Tuesday, October 01, 2013

(News) Tembea, Kimbia au Dhamini – Shiriki katika Rotary Dar Marathon 2013

Kimbia, Tembea au Dhamini – karibuni sana kudhamini mbio na matembezi haya ya hisani yajulikanayo kama Rotary Dar Marathon yatakayofanyika Jumatatu ya Oktoba 14 mwaka 2013. Lengo ni kuchangisha fedha zitakazotumika katika ujenzi wa maktaba ya kisasa yenye eneo la mita za mraba 800 katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Sambamba na maktaba iliyopo, ukarabati huu utazingatia uwazi, sanaa, ziara mafunzo, upatikanaji kwa wenye ulemavu na huduma za elektroniki – haya yote yatachochea maingiliano, mijadala na nyenzo za mafunzo shirikishi zitakazowawezesha viongozi wetu wa kesho.
 Mbio za hisani za Rotary Dar Marathon ni moja kati ya shughuli za uchangishaji fedha zenye mafanikio makubwa zaidi nchini. Mbio za mwaka 2011 na 2012 zilichangisha zaidi ya dola za kimarekani 840,000 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na ujenzi wa wodi ya wagonjwa wa saratani kwa watoto katika hospitali ya taifa ya Muhimbili iliyopo jijini Dar es salaam. Wodi hiyo ni ya kwanza kwa ubora Kusini mwa Jangwa la Sahara. Tanzania ni mimi na wewe katika kuijenga Tanzania yetu. Mchango wako utawezesha kutimiza lengo la ujenzi wa maktaba ya kisasa. Kwa maelezo zaidi au kujisajili, tafadhali tembelea tovuti ya Rotary Dar Marathon www.rotarydarmarathon.com 

No comments: