Rapper mwenye uwezo mkubwa wa kutumia lugha mbili ‘bilingual’ Webiro
N. Wasira maarufu kama Wakazi amesema video ya wimbo wake ‘Touch’ iko
tayari na anajiandaa kuiachia ili watu waweze kuiona akianza na watu
wake wa karibu na wadau wa media.
Wakazi amefunguka katika kipindi cha ‘The Chat’ cha 100.5 Timesfm
kinachoendeshwa na Ezden Jumanne a.k.a Ezden The Rocker Jumamosi saa nne
kamili asubuhi hadi sita kamili mchana.
Wakazi ameielezea kwa ufupi video yake kuwa ni video nzuri na kwamba
kazi waliyoifanya ni kubwa na kwamba hatawaangusha fans wake. “ The
video is nice and I’m happy kwa sababu tulifanya kazi ya ziada and the
song is doing well and shout out to Timesfm kupitia ‘The Chat’, na watu
wote wanaousikiliza wimbo na kuupenda pia.
Source: TimesFM
No comments:
Post a Comment