22.11.13

Thursday, November 07, 2013

BIOGRAPHY: Namtambulisha kwenu video model CUTE BINAH mrembo aliyeipendezesha video ya PHD "REST OF MY LIFE"

 Sabrina Abdul ndilo jina alilopewa na wazazi wake lakini yeye hupenda kujiita CUTE BINAH, ni mtoto wa kwanza katika familia yake kati ya watoto wawili waliozaliwa na mzee Abdul. Sabrina na video model ambaye anapenda sana kazi hiyo na mbali na kuwa video model tu huwa anafanya kazi zake nyingine ndogo ndogo zakusukuma maisha.

 Unaweza kujiuliza mtoto huyu mkali ameonekana wapi au unaweza ukawa umemuona lakini usikumbuke ni video gani umemwona ya msanii wa hapa Tanzania. Basi bwana huyu mrembo anaonekana kwenye video mpya ya HEMEDY PHD wimbo wake wa REST OF MY LIFE. Mwanadada amecheza part yake vizuri kabisa na asilimia 80 ameifanya video ile kuonekana nzuri kabisa.
Kama utabishana na mimi hebu fanya mpango wakubonyeza hii link ya video hiyo halafu utanipa jibu http://www.youtube.com/watch?v=fphCCywaunk

 Nilimuuliza Sabrina kwa mara ya kwanza wazazi kuiona video hii walisemaje na yeye alinijibu ya kuwa aliwaaga kuwa anaenda kushoot video so haikuwa ngumu sana walipoiona halafu isitoshe ile ndio kazi anayoipenda.
Nilimuuliza swala la usumbufu wa wanaume toka alivyoonekana kwenye hiyo video ya Hemedy au labda kama rafiki yake wakiume alimaindi akanijibu rafiki yake wakiume anatambua kama ile ni kazi kwahiyo hawezi maindi ila kusumbuliwa na wanaume ni kawaida mimi ni mtoto wa kike halafu isitoshe ni mzuri najitambua.

1 comment:

Michael Patrick said...

yes yupo mzuri sana big up