22.11.13

Tuesday, November 19, 2013

(News) Dar, Pwani wakabidhiwa bodaboda zao

 Mshindi wa Pikipiki katika Promosheni ya Timka na BodaBoda inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Bi.Hellen Kilawe akionyesha namba ya pikipiki aliyokabidhiwa na Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Bw.Matina Nkurlu. Katika Hafla ya kukabidhi pikipiki kwa washindi wa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. Jumla ya pikipiki 25 na fedha taslimu zilikibidhiwa kwa washindi hao. Wanaoshuhudia ni washindi wengine wa promosheni hiyo. Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.

 Mshindi wa Pikipiki katika promosheni ya Timka na Boda Boda inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Bw.Shadrack Moses  Pamoja na Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo,Bw.Matina Nkurlu wakihakiki kadi  ya pikipiki wakati wa makabidhiano yaliyofanyika katika Stoo za ofisi hiyo zilizoko Shekilango jijini Dar es Salaam. Pikipiki 25na fedha taslimu zilikabidhiwa kwa wakazi wa Dar es Salaam na Pwani. Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.

 Mshindi wa Pikipiki katika Promosheni ya Timka na BodaBoda inayoendeshwa na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Bw.Joseph Mambo akionyesha namba ya pikipiki aliyokabidhiwa na Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Bw.Matina Nkurlu. Katika Hafla ya kukabidhi pikipiki kwa washindi wa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. Jumla ya pikipiki 25 na fedha taslimu zilikibidhiwa kwa washindi hao. Wanaoshuhudia ni washindi wengine wa pikipiki hizo. Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.

 Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu(kulia)akimfungia kamba ya kofia ngumu”Helmet”Mshindi wa Promosheni ya “Timka na BodaBoda Bw.Joseph Mambo, Katika Hafla ya kukabidhi pikipiki kwa washindi wa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. Jumla ya pikipiki 25 na fedha taslimu zilikibidhiwa kwa washindi hao.anaeshuhudia kushoto ni Ofisa huduma za ziada wa kampuni hiyo Rashid Maggid.Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.

 Mshindi wa Pikipiki katika Promosheni ya Timka na BodaBoda inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Bi.Aziza Suleiman akipanda kwenye pikipiki yake aliyoshinda katika promosheni hiyo huku akisaidiwa na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina nkurlu(kulia)wakati wa Hafla  ya kukabidhi pikipiki kwa washindi wa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. Jumla ya pikipiki 25 na fedha taslimu zilikibidhiwa kwa washindi hao. Wanaoshuhudia ni washindi wengine wa pikipiki hizo. Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.

Mshindi wa Pikipiki katika Promosheni ya Timka na BodaBoda inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Bi.Aziza Suleiman akipunga mkono wakati akiondoka na pikipiki yake mara baada ya kukabidhiwa na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina nkurlu(kushoto)wakati wa Hafla  ya kukabidhi pikipiki kwa washindi wa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. Jumla ya pikipiki 25 na fedha taslimu zilikibidhiwa kwa washindi hao. Wanaoshuhudia ni washindi wengine wa pikipiki hizo. Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.

·        Washindi 25 wa Timka na Boda Boda.
·        Washindi 12 walamba Milion kumi na sita
·        Neema zaidi kuendelea kumiminika.
Dar es Salaam, 19th Novemba, 2013….Baada ya washindi zaidi ya 125 kujishindia Boda Boda na wengine kuendelea kujishindia fedha taslimu kila siku kutoka kampuni ya simu ya Vodacom ambazo ni zaidi ya milioni 430 zilizotengwa ndani ya siku 100. Vodacom Tanzania kwa mara nyingine tena  katika kuhakikisha inabadili maisha ya kila mteja wake imekabidhi Boda Boda kwa washindi 25 ambao ni wakazi wa mkoa Dar Es Salaam na Pwani.
Meneja Uhusiano wa Umma Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu amewashauri watanzania wote kuzidi kuendelea kushiriki katika promosheni hiyo inayoendelea kwa kasi zaidi ya miezi mitatu. Aliendelea na kusisitiza kuwa Kampuni yake imejidhatiti kuhakikisha haipo mbali na wateja wake kwa kuendelea kuwanufaisha kwa kuwapa Boda Boda ambazo zitakuwa ni si tu kuwasaidia kwa usafiri bali  ni msingi mzuri katika kuendeleza biashara zao.
”Kampuni yetu ipo kumnufaisha kila mmoja na imepania vikali kuhakikisha kila mtanzania anapata msingi ambao anaweza kutumia katika kuendeleza biashara zao, kwani siku hizi biashara ya Boda Boda imekuwa ni mwokozi kwa walio wengi ambao huongeza kipato chao kupitia biashara hiyo na ndio maana sisi Vodacom tumetenga piki piki zenye gharama ya kitanzania shilingi bilioni 1 kwaajili ya wateja wetu wote nchini” alisema Matina
Akiongezea kuwa “Kila mmoja anatamani kuwa na msingi ambao utamuwezesha aweze kuwa na biashara yake ambayo itamuingizia kipato matokeo yake kujikwamua katika hali ya kiuchumi, hivyo basi ni wakati wa kila mmoja kunufaika na promosheni mbali mbali zinazazotolewa na kampuni yetu, na ningependa kuendelea kuwashauri wateja wote wanaoshiriki na wanaoanza kushiriki kuzidi kuendelea kwani ni haki ya kila mtanzania kujishindia boda boda kutoka Vodacom”
Ili kuweza kuwa mmoja kati ya washindi kutoka promosheni hiyo ya Timka na Boda Boda ni rahisi sana, wateja wote wa Vodacom wanatakiwa kushiriki kwa kuandika neno PROMO na kutuma kwenda namba 15544.
Mwisho.

No comments: