Monday, November 18, 2013

(News) JAMBO SQUARDS NA LADY FIRE WATISHIWA KUUAWA NA MTU ANAYEJIITA KAKA KIBO WA ARUSHA

Kuanzia kushoto ni Nigger C, Ordinally na Lady Fire

Exclussive akiongea na DjHaazu wa MJ FM Arusha mmoja kati ya member wanaounda kundi la Jambo Squard NIGGER C a.k.a Chaalii Mtoto wa bibi amefunguka kuhusu wao kutishiwa Kuuwawa na mtu ambaye anajihisi kuwa yeye ndiye Wamemuimbia wimbo unaokwenda kwa jina la KAKA KIBO ambapo ngoma hiyo ilitungwa na Vijana hao na kupewa nafasi ya kuiimba Mdogo wao anayejulikana kwa jina la Lady Fire Manzi ya Ara.
 Nigger C amesema baada ya wimbo huo kuanza kufanya poa kwenye Vituo kadhaa vya radio Nchini hatimaye ametokea Mtu ambaye anadai kuwa wao wamemuimbia yeye na vitu vyote vilivyoimbwa vinamlenga yeye Direct na jina lake ni Kibo na huyo mtu alishawahi kujiita yeye ni manager wa Jambo kitu ambacho wao kiliwaudhi na hatimaye kumkataa na kukaa mbali naye ambapo kilichofuatia ni uhasama uliosababishwa na mtu huyo kuwashikia fedha zao million 3 akidai kuwa anawatengenezea future kibiashara huku akijitapa kuwa na mkwanja wa kutosha na mwishowe wasanii hao walipogundua ni mbabaishaji hatimaye walimbwaga na walipoulizia fedha zao jamaa aliwapa laki 8 tu kitu ambacho kiliwakera wasanii hao.

Nigger ameendelea kumiminika zaidi na kusema kuwa wamemrecord mtu huyo wakati akiongea na moja kati ya Viongozi wa GrandMaster record Studio ambayo wanafanyia kazi wasanii hao na sauti hiyo wanayo ya Kaka Kibo huyo akisema kuwa amewatafutia Majambazi vijana hao na amewalipa advance kwa ajili ya kuwalima risasi vijana wa Jambo Squard ambao ni Nigger C na Ordinally a.k.a Kisu kikali a.k.a Jogoo Kichaa na pia kumkata miguu na mikono Mwanadada Lady Fire.

Hata Hivyo wamewaahidi wananchi Kufikisha Sauti hiyo Radioni Leo Jumatatu Na watu watamsikia Mtu huyo akitiririka akiamini kiongozi huyo atakuwa upande wake bila kujua kwamba anarecordiwa na Kiongozi huyo hayuko tayari kuwasaliti vijana wake kisa fedha za mtu huyo.

Jambo Squard wanasema kinachowauma zaidi ni kwamba mtu huyo anasema atasambaza fedha kwa MaDJ na Mapresenter ili ngoma za jambo Squard zisipigwe na kwamba kuna kituo kimoja cha Radio arusha ambacho kimeandika Tangazo kabisa ukutani ukiingia studio kwao kwamba wimbo wa jambo squard usipigwe....

Nigger C amesema hadi sasa wao wanafuatilia RB Kumkamata mtu huyo ambaye inasemekana ana Mabov ya kutosha kumwaga ila wao wanaamini kama YAHAYA aliimbwa na JD na hakumshtaki JD inamaanisha kuwa walikuwa wengi na wao wanawajua Kibo wengi.

MSIKILIZE NIGGER C AKIONGEA NA DJHAAZU HAPA CHINI
KUSIKILIZA CLICK LINK HII >> http://old.hulkshare.com/ow4wkucz81ds

Ndani ya wimbo huo ameimbwa au wamefikishiwa ujumbe watu ambao wanapenda kujioshea au kujibandika vyeo wasivyostahili mfano kuna line inasema " Eti anasema ni Maneger wa Jambo"

SIKILIZA WIMBO HUO KAKA KIBO WA LADY FIRE AKIWASHIRIKISHA JAMBO SQUARDS NA RAMA B  HAPA CHINI

FUATILIA HAPA HAPA KITAKACHOENDELEA

No comments:

Post a Comment