Meneja
wa Vodacom Moshi Michael Kambi (kulia) akimkabidhi wakala wa M-pesa wa
mjini Moshi Anna Theobald mfano wa ujumbe wa simu unaomjulisha
kupokea Sh 100,000 kwa njia ya M-pesa kutokana na ushindi kupitia droo
ya promosheni ya
Mkwanja kwa Wakala inayoendeshwa na Vodacom kwa mawakala wa M-pesa nchi nzima. Anna ni mfanyabishara wa duka la vipodozi mjini humo.
Wakala
wa M-pesa Mjini Moshi Kudra Shwaibu akipokea kutoka kwa Meneja wa
Vodacom Moshi mfano wa ujumbe wa simu unaomjulisha kupokea Sh 100,000
kwa njia ya M-pesa kutokana na ushindi kupitia droo ya promosheni ya Mkwanja kwa Wakala
inayoendeshwa na Vodacom kwa mawakala wa M-pesa nchi nzima. Kudra ni
mfanyabishara wa Saluni ya kiume iliyopo Mabogini mjini humo ambayo
huitumia kuendeshea
biashara ya uwakala wa M-pesa
Zamzam
Mohammed(kulia) ambae ni wakala wa M-pesa Mjini Moshi akifurahia
kupokea mfano wa ujumbe wa simu alioupokea kumjulisha kupokea Sh 100,000
za ushindi wa droo ya promosheni ya Mkwanja kwa Wakala inayoendeshwa na Vodacom nchi nzima. Anaemkabidhi ni Meneja wa Vodacom Moshi Michael Kambi .
Meneja
wa Vodacom Wilaya ya Missungwi Mkoani Mwanza Gift Tesha (kushoto)
akimkabidhi cheti cha ushindi wakala wa M-pesa Juliana Sylvanus
alichopatiwa
na Vodacom kutokana na kuibuka mmoja wa washindi wa droo ya promosheni
ya Mkwanja kwa Wakala inayowahusisha mawakala wa M-pesa nchi nzima. Hadi sasa zaidi ya mawakala 1350 wameshinda fedha taslimu kutoka Vodacom.
Mawakala
wa M-pesa nchi nzima wameendelea kujishindia zawadi za fedha taslimu
kupitia promosheni ya Mkwanja Kwa Wakala inayoendeshwa na Vodacom kwa
shabaha ya kuwawezesha mawakala wake hao kuwa na sababu nyengine ya
kufurahia kuwa sehemu ya mafanikio makubwa ya huduma ya M-pesa hapa
nchini.
Zaidi
ya mawakala wa M-pesa 1,350 kutoka mikoa yote wameshajishindia zaidi ya
Sh. 135 Milioni katika promosheni hiyo iliyobakisha wiki tatu kufikia
ukomo wake baadae mwezi ujao.
“Promosheni
inakwenda vizuri na kikubwa zaidi mawakala wetu wameipokea na
kuifurahia sana, hili ndilo haswa lililokuwa lengo letu.”Alisema Meneja
Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim
Mwalim
aliongeza kuwa “Tunawatembelea washindi wote popote pale walipo iwe
mjini au kijijini na kukaa nao na kupitia kwao wanatupatia mawazo mengi
mazuri ya namna ya kuboresha huduma yetu hii ambayo kwa sasa imekuwa
mkombozi mkubwa kwenye maisha ya watanzania.”
M-pesa
ina mawakala zaidi ya 55,000 nchi nzima na kuwa huduma pekee ya miamala
kwa njia ya simu za mkononi yenye mtandao mkubwa zaidi wa mawakala
na hivyo kuwa huduma inayoongoza kwa kufikiwa kwa urahisi na kwa
ukaribu zaidi na watanzania mijini na vijijini.
Ili
wakala wa M-pesa aweze kuingia kwenye droo ya kila wiki anapaswa kuwa
amefanya miamala isiyopungua mitano kwa siku. Mawaka 270 hujishindia Sh
100,000 kila mmoja kwenye droo hizo zinazosimamiwa na bodi ya michezo
ya kubahatisha.
Kupitia
M-pesa mteja wa Vodacom anaweza kufanya miamala na zaidi ya biashara
350 ikiwemo kununua tikiti za ndege, kulipia ada, kutoa au kuweka fedha
kwenye akaunti ya benki za biashara zaidi ya 15, kulipia kodi TRA,
kununua muda wa maongezi wa hewani, kulipia huduma za ving’amuzi vya
televisheni, kununua luku, kulipia huduma za maji n.k.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment