Meneja Uhusiano wa
Umma wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu(kushoto)akiwa pamoja na Ofisa wa bodi
ya michezo ya kubahatisha Bakari Abdallah,Ofisa huduma za ziada wa Vodacom
Rashid Maggid huku Kaimu mkuu wa kanda ya Kaskazini wa Kampuni hiyo Bi.Assumpta
Malongo wakihakiki mmoja ya namba ya simu ya
washindi wa Promosheni ya “Timka na BodaBoda” iliyofanyika katika kituo
cha radio cha Sunrise mjini Arusha juzi.Jumla ya washindi(95)wamejishindia
Bodaboda na(55)wamejinyakulia fedha taslimu.Ili kujiunga na Promosheni hiyo
tuma neno Promo kwenda 15544.
Baadhi ya washindi wa
Promosheni ya “Timka na BodaBoda”inayoendeshwa na Vodacom Tanzania wa mkoa wa
Arusha na Kilimanjaro wakiondoka na Bodaboda zao baada ya kukabidhiwa rasmi
jana jijini humo.Jumla ya washindi(95)wamejishindia Bodaboda na(55)wamejinyakulia
fedha taslimu.Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.
Mshindi wa Promosheni
ya”Timka na Bodaboda”inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,Elinipa Mmari akinesha
namba mpya ya pikipiki yake baada ya kukabidhiwa na Kaimu Mkuu wa kanda ya
Kaskazini wa Kampuni hiyo Bi.Assumpta Malongo(kushoto)katikati ni mume wa
mshindi huyo Alfred Mmari. Jumla ya washindi(95)wamejishindia Bodaboda
na(55)wamejinyakulia fedha taslimu.Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.
Meneja Uhusiano wa Umma
wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu(kulia)akimfungia kamba ya kofia
ngumu”Helmet”Mume wa mshindi wa Promosheni ya “Timka na BodaBoda mkazi wa Siha
mkoani Kilimanjaro Alfred Mmari,kushoto ni
Kaimu Mkuu wa kanda ya Kaskazini wa Kampuni hiyo Bi.Assumpta
Malongo(kushoto)katikati ni mume wa mshindi huyo Alfred Mmari. Jumla ya
washindi(95)wamejishindia Bodaboda na(55)wamejinyakulia fedha taslimu.Ili
kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo
kwenda 15544.
Kaimu Mkuu wa kanda ya
Kaskazini wa Vodacom Tanzania Bi.Assumpta Malongo(kulia)akimkabidhi funguo ya
pikipiki yake mshindi wa Promosheni ya”Timka na Bodaboda”Paulo Kivuyo mkazi wa
njiro.Jumla ya washindi(95)wamejishindia Bodaboda na(55)wamejinyakulia fedha
taslimu.Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.
Meneja Uhusiano wa
Umma wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu(kushoto)pamoja na Kaimu mkuu wa kanda
ya Kaskazini wa Kampuni hiyo Bi.Assumpta Malongo,wakimshuhudia mshindi wa
Promosheni ya”Timka na Bodaboda”Bw.Paulo Kivuyo wa Arusha akiwasha pikipiki
yake mara baada ya kukabidhiwa rasmi jijini Arusha jana. Jumla ya
washindi(95)wamejishindia Bodaboda na(55)wamejinyakulia fedha taslimu.Ili
kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo
kwenda 15544.
Kaimu mkuu wa kanda ya
Kaskazini wa Vodacom Tanzania Bi.Assumpta Malongo,akimshuhudia mshindi wa Promosheni ya”Timka na Bodaboda”Bi.Elinipa
Mmari akiwa amepakizwa na mumewe Alfred Mmari mara baada ya kukabidhiwa rasmi jijini Arusha
jana. Jumla ya washindi(95)wamejishindia Bodaboda na(55)wamejinyakulia fedha
taslimu.Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.
Katika
hali ya kushangaza wengi wakazi wa Arusha na mkoa wa Kilimanjaro, wanaoongoza
kwa kuzoa Boda Boda nyingi katika promosheni ya Timka na Bodaboda inayoendeshwa
na kampuni ya mawasiliano inayoongoza nchini Vodacom ambapo ikiwa ni siku 20 tu
tangu kuanza kwa promosheni hiyo tayari jumla ya boda boda 29 zimenyakuliwa na
wakazi wa mikoa hiyo.
Boda
Boda hizo ambazo tayari zimepelekwa jijini humo kwa ajili ya kukabidhiwa kwa
washindi zimeendelea kuvutia hisia za wakazi wa mikoa hiyo na kuzua gumzo kila
upande juu ya washindi waliopatikana kutoka katika mkoa huo ambapo wengi
waliamini kuwa Promosheni hizo hufanyika kwa Dar es Salaam tu.
Akizungumza
wakati wa kuwakabidhi washindi pikipiki wa mikoa hiyo,Meneja Uhusiano wa Umma
wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu amesema wameshangazwa na ushindi mkubwa ambao
wameupata wakazi wa kanda ya kaskazini .
“Watu
wengi huwa wanaamini kuwa kila promosheni tunayoifanya huwa ni kwa wakazi wa
Dar es Salaam tu hili si kweli kwani Wakazi wa Arusha na Kilimanjaro wamedhihirisha
hili kwa kuutoa mkoa wao kimasomaso kwa kujizolea bodaboda 29 na bado ziko
zaidi ya pikipiki hizo 370 ambazo zinaendelea kushindaniwa,” alisema Nkurlu na
kuongeza.
“Tumeanza
na wakazi wa Arusha na tutaenda pia katika mikoa mingine lengo letu sisi kama
Vodacom ni kuhakikisha tunaendelea kuboresha na kuimarisha maisha ya wateja
wetu ambao wamekuwa wakituunga mkono siku zote, Tunaamini kuwa kwa kuboresha
maisha ya wateja wetu kutoka katika faida tunayoipata ili kuwawezesha wao
kuendelea pia kutuunga mkono siku hadi siku na kwa nguvu zaidi,” alisema.
“Sasa
hivi sehemu nyingi za Tanzania wakazi wengi wanapata tabu ya usafiri na usafiri
rahisi kwa sasa ni pikipiki maarufu kama Bodaboda, gharama za maisha zimepanda
sana usafiri pia umekuwa tabu, hivyo tumeona vyema sasa kuwapatia wateja wetu
nafasi ya kujishindia usafiri ambao unatumia gharama nafuu,”
Nkurlu
amesema jambo la msingi ni kuhakikisha tunawezesha ndoto za watanzania wengi
kumiliki usafiri wao, na hata kwa wale ambao wanapenda kuwa wajasiriamali basi
hii ni fursa ya kipekee kujishindia Bodaboda hizi.
Akizungumza
baada ya kukabidhiwa zawadi ya bodaboda mume wa mshindi wa boda boda,Elinipa
Mmari,Bw Alfred Mmari, alitoa wito kwa wanaume,kutowakataza wake zao,kucheza bahati nasibu ya timka na
boda boda kwani ina manufaa makubwa.
“mimi
nilikuwa namkataza mke wangu, kucheza lakini baada ya ushindi huu,natoa wito
kwa wanaume wenzangu kuwaacha wake zao kucheza na hata kuwasaidia kwani
wanabahati ya ushindi”alisema Mmari
Katika
hafla hiyo, iliyofanyika viwanja vya Sanawari,mfanyabiashara Paulo Lairumbe
kivuyo,mkazi wa Njiro Arusha pia alikabidhiwa boda boda yake aliyeshinda.
Katika
Promosheni hii ya Timka na Boda Boda kampuni
ya Vodacom imetenga jumla ya bodaboda 430 kwa kipindi cha siku 100. Ili kupata
nafasi za kujishindia bodaboda hizo, na shilingi milioni moja kila siku mteja
wa Vodacom atatakiwa kutuma ujumbe wenye neno PROMO kwenda 15544.
Mwisho...
No comments:
Post a Comment