22.11.13

Wednesday, November 13, 2013

(News) NAVY KENZO Introducing ‘CHELEWA’ November 14, 2013.

 Navy Kenzo ni kundi linaloundwa na vijana watatu; Haika, Nahreal na Weastar ambao wameshawahi kutamba na ngoma kama Kizembe, Usinibwage, Naomba Uniroge, n.k. siku ya alhamis tarehe 14 November 2013 wanatarajia kuachia ngoma yao nyingine.
“CHELEWA” ndio jina la ngoma hiyo yenye mahadhi ya Afro-pop yenye kuelezea watu wawili waliokaa kwenye mahusiano kwa muda mrefu bila kufunga ndoa hali inayomfanya msichana aone kama mvulana wake anachelewa kufunga pingu za maisha.
Ngoma hii imepikwa chini ya producer ambaye pia ni msanii wa kundi hilo, Nahreal kupitia HomeTown Record. “Ni ngoma moja ya tofauti sana ambayo nadhani wengi watafaifahamu Navy Kenzo inafanya nini na watu wa aina gani, so watu wasubiri ujio wa tofauti kabisa kutoka kwa Navy Kenzo.” – Haika.
 

No comments: