Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Bw.
Yusuph Mwenda(katikati) akisikiliza jambo toka kwa Ofisa Mkuu wa kitengo
cha Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Bw.Hassan Saleh(kulia) muda
mfupi kabla ya kuzindua rasmi duka
jipya la Vodacom lililopo Shamo Tower Mbezi beach gorofa ya kwanza jana jijini Dar es
Salaam.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Bw. Yusuph Mwenda akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa duka la
Vodacom Tanzania lililopo Shamo Tower Mbezi beach gorofa ya kwanza jijini Dar
es Salaam,wengine kulia ni Meneja wa duka hilo,Bw.Kartic Subramaniam na kulia
ni Ofisa Mkuu wa kitengo
cha Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Bw.Hassan Saleh.
Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Bi.Pendo Richard
(kulia) akimuelezea Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph
Mwenda matumizi ya baadhi ya bidhaa zinazopatikana katika duka jipya la kampuni
hiyo,Mara baada ya Meya huyo kuzindua duka hilo jana Shamo Towers gorofa ya
kwanza, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. Katikati ni Ofisa Mkuu wa kitengo cha Mauzo na
Usambazaji wa kampuni hiyo,Bw. Hassan Saleh.
· Upatikanaji
wa huduma za Vodacom wazidi kurahisishwa
Dar Es Salaam
17 Novemba 2013… Katika kuhakikisha inakidhi mahitaji ya wateja wake na
kuwaridhisha kwa kile wanachokihitaji, Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza
Tanzania Vodacom imezindua duka jipya ambalo litawawezesha wateja mbalimbali wa
kampuni hiyo wakiwemo wakazi wa Mbezi Beach kunufaika na upatikanaji wa karibu
wa huduma mbalimbali za muhimu za mawasiliano.
Mgeni rasmi
katika ufunguzi huo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda
amewaasa wakazi wote wa Mbezi kutumia ipasavyo duka hilo ili kuweza kutatua
matatizo yao ya huduma za kimawasiliano.
”Najua walio
wengi walikua wakisubiria na kutamani kuona ni muda gani Vodacom itawaletea
duka ambalo litawapa huduma mbali mbali za kimawasiliano, sasa kuanzia leo duka
limefunguliwa rasmi hivyo mnapaswa kulitumia ipasavyo kwani limewekwa hapa
kwaajili yenu wote wateja wa Vodacom”. Alisema
Mwenda
aliongeza kuwa “Idadi kubwa ya watanzania ambao ni watumiaji wa huduma za
kimawasiliano imekuwa ikiongezeka siku hadi siku, hivyo kufuatia uzinduzi huo
itakuwa ni suluhu tosha ya kuwawezesha wateja walioko Mbezi Beach na hata nje
kuweza kutatua haja zao pale wanapokuwa wanahitaji huduma”.
Kwa upande
wake Ofisa mkuu wa kitengo cha Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Hassan
Saleh amesema kampuni yake inatambua mchango unaoendelea kutolewa na wateja
wake, hivyo inazidi kuwaunga mkono kwa kuwapa urahisi wa upatikanaji wa huduma
kwa kuwafungulia duka ambalo litawawezesha wakazi wa Mbezi kutokupoteza muda
wao mkubwa kwenda mbali kwaajili ya huduma mbalimbali za Vodacom, badala yake
kutatua matatizo yao hapo hapo Mbezi Beach katika duka hilo.
“Mahitaji ya
huduma kwa wateja sasa ni makubwa na watanzania wanahitaji kupata kile
watakachokifurahia katika maisha yao ya kila siku. Hivyo Vodacom kupitia duka
hilo itawawezesha wakazi wa Mbezi na maeneo mengine kuwa karibu na upatikanaji
wa huduma na kuacha kwenda mbali kama walivyokuwa wakifanya apo awali” Alisema
Saleh
Akiongezea
kuwa “Bado tutaendelea kurahisisha upatikanaji wa huduma zetu kwa kuzidi
kufungua maduka mengi zaidi sehemu mbalimbali ambazo hazijafikiwa na
kuhakikisha wateja wetu wote wanaendelea kufurahia huduma zetu za Vodacom,
hatimaye kuendelea kubaki kinara kwa kuwapa huduma bora wateja wetu”
Hadi sasa
Vodacom inamiliki maduka 72 yaliyo katika sehemu mbalimbali za nchi ambayo
yanaendelea kutoa huduma bora na zinazostahili kwa wateja wake kitendo ambacho
kinawafanya kuwa ni kampuni inayoongoza hapa nchini.
Upanuzi huu wa wigo wa huduma za mawasiliano
ya simu wa Kampuni ya Vodacom Tanzania unafuatia uwekezaji kwenye mfumo wa
mawasiliano wa 3G na 4G mfumo ambao unaotumia teknolojia mpya ya mawasiliano
kazi iliyofanywa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania.
Mwisho…
No comments:
Post a Comment