22.11.13

Wednesday, November 13, 2013

(News) WATANZANIA WANUFAIKA NA AJIRA KUPITIA M-PESA

 Meneja wa Vodacom Ubungo Asajile Mwakisunga (kulia) akimkabidhi Regina Xaver cheti cha ushindi wa uwakala bora wa M-pesa baada ya kupitia promosheni ya Mkwanja kwa Wakala inayoendeshwa na Vodacom kwa mawakala wa M-pesa nchi nzima. Regina alizawadiwa pia Sh 100,000. Zaidi ya Mawakala 1080 wameshashinda fedha taslimu na vyeti kupitia promosheni hiyo hadi sasa.

 Meneja wa Vodacom Mtwara Mjini Charles Minungu (Kulia) akimkabidhi wakala wa M-pesa Yazidu Abdala cheti cha ushindi wa uwakala bora kwa Mtwara Mjini kupitia promosheni ya Mkwanja kwa Wakala inayowahusisha mawakala wa M-pesa nchi nzima. Yazidi alipatiwa pia Sh 100,000. Anaeshuhudia ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kusini Henry Tzamburakis.  Zaidi ya Mawakala 1080 wameshashinda fedha taslimu na vyeti kupitia promosheni hiyo hadi sasa.

Eligen Andrew Zongo Wakala wa Mpesa Ubungo, Dar es salaam akipokea kutoka kwa Meneja wa Vodacom eneo la Ubungo Asajile Mwakisunga cheti cha Uwakala Bora wa M-pesa pamoja na mfano wa hundi ya Sh 100,000 alivyoshinda kupitia promosheni ya Mkwanja kwa Wakala inayowahusisha mawakala wa M-pesa nchi nzima. Zaidi ya Mawakala 1080 wameshashinda fedha taslimu na vyeti kupitia promosheni hiyo hadi sasa.

No comments: