22.11.13

Friday, August 07, 2009

PLANET BONGO & 5 CONNECT.

Niaje watu wangu, leo kama nimefanyiwa mahojiano na kituo cha East Africa Televishen, asubuhi nilifanya enterview na kipindi cha 5 Connect kinachorushwa kila jumatano saa moja hadi saa mbili usiku. Enterview hii ilikuwa inaongelea utandawazi wa network hapa kwetu bongo, kumekuwa na blog nyingi je tunafaidikaje sisi wana libeneke. Kama upo bongo cheki jumatano ya wiki ijayo uone yaliyomo.

Ilipofika majira ya mchana nikafuatwa na mzee wa Planet Bongo Dullaaaaah, huyu jamaa bwana alikuja na topic yake inayosema wasanii kupanda na madj wao stejini mbona hapa kwetu wasanii wengi hawana madj wao. so mimi nilikuwa natakiwa kuyajibu hayo maswali na kuonyesha uzohefu wangu wa kubackup na kushika mashine nikiwa stejini. Angalia Planet Bongo jumatano ya wiki ijayo halafu tuoneeeee.

Camera man namba 1 pale EATV, anajulikana kwa jina la Tawakal, huyu ndio aliyekuwa anatuuzisha sura na kucheza na maujanja yote.

Msanii mdogo mwenye uwezo wa kurap nae alikuwa anaojiwa siku ya leo, anaitwa Yang Dee, halafu soon naipandisha video yake mpya ya Teacher.

Dullah mtangazaji wa kipindi cha Planet Bongo, Tawakal mpiga picha na dj choka mkali anayechipukia.

No comments: