CPWAA'S PRE-LAUNCH PARTY.

Thursday, December 03, 2009

Websites launch, Company launch, Clothes launch, Documentary, Xclusive performance,
New song and Video Premier.
Date: 8Th Dec 2009 From 9.00 pm for 15000/= ONLY!

NJOO UJIONEE WATOTO WA KINAIJA NA WAKITANZANIA.

THE MAKING VIDEO YA MANGWEAR "CNN"

Jana majira ya jioni pale maeneo ya Shopperz Plaza kwenye club ya RUNWAY ndipo palipofanyika video mpya ya Mangwear inayoitwa CNN. Washkaji walikuwa kibao cha ajabu kuna watu waliniomba niwapige picha ila nisiandike majina yao.
Video hii imetengenezwa na kampuni ya Kallage's Picture

Aliyesimama ni Kallage mwenyewe akiwaelekeza jambo la kufanya

Uhondo wa ngoma uingie kati ucheze..dada huyu aliona hapana ngoja nijivute tu mbele.

Dully uzalendo ulimshinda ikabidi nae ashuke

Ndugu yetu Romeo Jons nae hakuwa nyuma

Kallage akiwaonyesha baadhi ya vipande.

Dada yetu mrembo

Dully na Dagma aka 120

Miraji Kikwete na dj choka

Babuu wakitaa na watoto wakali.

flowers

Ndugu yangu Adamu utaliweza hilo chupa

RAS NAS ndani ya Sri Lanka

Ras Nas pamoja na kikosi chake wakiwasili Colombo leo (Jumatano) tayari kwa maonyesho matatu miji ya Colombo na Galle, Sri Lanka, wikiendi hii. Ras Nas anawasilisha Norway na Tanzania vile vile!

Toka kushoto Larry Skogheim (besi, Norway), Ras Nas aka Nasibu Mwanukuzi (sauti na ridhim gitaa, Tanzania), Dag Pierre (solo gitaa, Sweden), Chuck Frazier (solo namba mbili, Houston Texas), Uriel Seri (drums, Ivory Coast), Karlos Rotzen (kinanda, Martinique).

NYIMBO MPYA ZILIZOTUFIKIA.

Ya kwanza nikutoka kwa mzee wetu Zahir Ally Zorro na wimbo wake mpya unaoitwa BARUA PEPE akiwa amemshirikisha mwanadada Stara Thomas.

Wa pili ni kutoka kwa Chidi Beenz na wimbo wake unaitwa CHAGUO LANGU, amefanyika katika studio ya Fishcrab producer akiwa ni Lamar.

Wimbo wa tatu nikutoka kwa O Ten wimbo unaitwa NAFUNIKA amewashirikisha wasanii wenzake Squeezer na Domokaya, wimbo huu umetengenezwa na studio inayoitwa MPOAFRICA

KUTOKA KWENYE FACEBOOK YA LADY JD, Video ya Teja ime leak

Wednesday, December 02, 2009

Hii ni habari kutoka kwa mwanadada Lady JD "Video ya Teja ime LEAK wala sija Release, nashangaa ni nani ameamua kufanya hivyo? Yote kheri tutaendelea tu kukomaa mpaka tuone mwisho"

COVER ALBUM YA VETO.

TRAFFIC LIGHT PARTY.

BABY POWDER PREMIERE- (HOUSTON,TX)


Houston,TX THANK YOU so much for the love, our BABY POWDER HOUSTON premiere was SUPER GREAT, Would like to share this special moment with everybody.. On the other side PLEASE HELP us to pass this massage ,Due to the fact we still haven't secured a theater in Washington DC area JAKE PRODUCTIONS is sadly going to have BABY POWDER PREMIERE at a later date ( NOT DECEMBER 5TH 2009 AS PLANED) We are glad to announce that the other dates are still the same, in this case BABY POWDER premiere next stop is

WICHITA,KS ( DECEMBER 12th 2009)
WARREN THEATER
WEST SIDE

MINNESOTA,MN (DECEMBER 19th 2009)

Thank you

Jake Productions

Message kutoka Bano to all his fans baada ya interview ya J Murder owner wa Tongwe Records Jumamosi on Bongo Flava.

Habarini ndugu zangu watanzania?
I hope kila mtu yu salama.Nimeamua kuchukua fursa hii kuongea na umma juu ya roumuz zinazo nikabili mimi.Ningependa watu waajue kuwa J-RYDA was a close friend of mine hata J-MURDA naye pia.I wonder why wameamua kunifanyia hivyo by this hour?TONGWE was facing a problem by the time producer wao DUKE anaondoka studio so they needed a producer & J-MURDA was a brother of my school mate so ikawa rahisi kunipata mimi.I started producing the songs tongwe kuanzia mwezi march mpaka july.Kukaanza kutokea matatizo baina yangu mimi na the owner coz alishindwa kunilipa pesa za matangazo ambazo zilikuwa zimebaki,tuligombana sana then nkaona ngoja nirudi nyumbani.Nikawa naenda studio when im needed nkawa sijiendei tu.By august nkaanza kumpeleka J-RYDA studio with our fellow producer named carson-g.By 26 of august me nkasafiri kuja kusoma which means me na j-ryda kama kukaa tongwe studio me na yeye its jus only 3 weeks ambazo in real sense hakuna production isiyozidi nyimbo 3 hata kama mtu una usongo gani u cant produce more than 3 songs pre 3 weeks.

Yeye kuclaim me nimeondoka nanyimbo zake its meaningless coz they know dat me nlikuwa nimeproduce nyimbo ngapi before mimi kuondoka tho by the time me naondoka ni nyimbo moja tu ''watoto wa mjini'' ya jos mtambo & chidi benz ndio iliyokuwa imetoka.Alaf ever since i started my music career sijawahi kutengeneza pesa yeyote ile kutoka kwenye music,so i hope u pipo can feel the feeling ambayo i am going through rightnow.

Tukiwa studio kuna vitu vingi sana vinatokea kwa mfano;u can make the whole song alaf ukamsikilizisha mwenzio akupe comments zake then maybe anakwambia the bass haijakaa vizuri then unamwambia put it the way u want,akishafanya then off u go.Sasa beat za style hii zipo nyingi sana ambazo me na RYDA tumefanya ever since kitambo till 2day.Angesema hizo ndio zake kidogo ningemuelewa but he did not do that.

Talking about goodboi,nimerudi ya cyrill and further songs kuwa they are not my art haya aseme but in heart he knows.Nikianza kugombania nyimbo ambazo they are about to fade out ni ujinga!!! kama anaclaim ameproduce si kuna nyimbo mpya ambazo yeye ameproduce do they vary na hizo ambazo nimeproduce?!!!!

Furthermore,alikuwa wapi kusema hivyo muda wote nyimbo zinatoka naenda kwenye interviews sometimes i even forget na ye huwa ananikumbusha dat yo boi u got these interviews and all dat.Siku ambayo me naondoka nakumbuka niliwatumia texts yeye na our other fellow CARSON -G dat i did not take them to the spot ambayo nlitaka tufike so they shud fight for that coz atleast mimi nimeweza kuwafungulia njia so it wili be easy for them to reach up.

3 weeks kabla ya leo ilininbox na kuanza kuniambia dat i think its time for him to go on alone with the music career so its like he duznt need me anymore.Ila kama ni goodtymes tule pamoja kama kawaida.The way nilivyomuelewa mimi its like alikuwa ananidump, nkamwambia poa.We were talking about so many things even future projects and all dat so dat means kulikuwa hamna tatizo lolote.

J`mosi ambayo wamefanya interview usiku wake we were on facebook chatin as if he did not do anything to harm me.Sunday nkaanza kupokea simu kutoka kwa watu tofauti wakiniambia about this,nkasema ngoja niulize imekuwaje.Nkampigia Cyrill and he told me the same thing,nkaongea na dozen ye ndio akaniambia dat they did the interview na wewe so dats why i decided to txt you.Niliongea na nick wa pili na watu kadhaa kila mtu akawa anashangaa.

Nway,

They shud come up with a new plan ya kuinyanyua studio but not kuwa mislead my pipo.And kuhusu nyimbo kudistribute online!
naomba wanitajie hizo webs ili nizidistribute kweli sasa without a doubt coz itakuwa haileti maana kama nikizificha tena.And i promise them kila baada ya siku 3 ntakuwa nazitoa kweli.Wanitajie web moja tu nifanye kazi yangu.
Kukaa kunipakazia vitu vya ajab ni si busara njema kwani ni kunidhalilisha na si kuniaibisha.Kama wanataka kunyanyua studio kwa style ya roumuz studio itakufa mapema sana.Alaf J-MURDA anasahau kwamba nilikuwa shule nkawa naproduce nilipohitajika shule nkaacha kuproduce which means hata RYDA nae atakuwa studio and then ataondoka kama nilivyofanya mimi.Wanatakiwa wafurahi kwamba i paved the way for them to succeed not to knock me down.

Sitatoa nyimbo hata moja ambayo nimefanya kuanzia 2007-09 so nawaruhusu wazitumie hizo nyimbo ambazo niliziacha zije kutoka baadae,wafute zile tags zangu zote waweke zao its okay i wont mind.I will just start a new page of my music career with not more than 50 songs to say goodbye to ma fans,my music career is over according to me.Sitaproduce anymore song zaidi ya hizo and i will just want to prove them wrong.NITAFANYA HIVI SI KWA KUTENGENEZA BATTLE WITH THEM BALI KWA KUWAFANYA WATENGENEZE VITU VIZURI KAMA VYANGU,KWANI WALIVIONA NI VIZURI NDIO MAANA WANAVIGOMBANIA.

Alaf i got a good msg for them, wasikilize lyrics zangu za nyimbo ya ''ON FIRE'' watajihisi niliwataja wao and its true coz i was prepared for this to happen 1 year ago.So i am forever prepared they shud get a new plan.Money its juss the other side of life so wasichanganyikiwe sana 200,000 kuna millions and billions watu wanashika na still they act cool.

Nawatakia kila la kheri katika maisha yao ya kimuziki.And thanks pia kwa watu wote watakao kuwa bega kwa bega na mimi katika hili.

Thanks to u once again,

Yours,
Bano Stylez Dha General.

NIMETIMIZA NDOTO YANGU YA KUTEMBEA NA FARASI.

Tuesday, December 01, 2009

Mwanadada Besta juzi kati ilikuwa siku yake yakuzaliwa, Besta anasema "nimetimiza ndoto yangu ya kuride a horse on my b,day! it was just a private party on a beach"

Hapa nikiwa juu ya farasi.

Nawapenda mashabiki wangu wote na msione kimya sana ujue kina mshindo,

MCHUMA WA LADY JAY DEE NDIO HUU.

Msanii wa bongo fleva anayemiliki band ya Machozi, Lady JD amenunua kitu cha Nissan Murano ndicho mchuma anaotembelea town kwa sasa. Kwa hapa kwetu gaari hizi zinahesabika kwa kweli, big up sister kazi zako tunazikubali.

WHO IS THE BEAUTY OF THE WEEK.

Monday, November 30, 2009

Anaitwa Teddy Kalonga, top model anayetesa kule kwa wenzetu na anaonekana sana kwenye video za wasanii wa kule ugaibuni.

Huyu anaitwa Cynthia Masasi kimwana toka pale jijini Mwanza ila kwa sasa makazi yake yapo nje ya nchi, pia huyu ni model mkubwa tu na alienda huko kitambo sana.

VOTE KWA YULE UNAYEMUONA ANAFAA KUWA BEAUTY KWA WIKI HII.

DJ CHOKA PRESENT HANDSOME OF THE WEEK.

Huyu ndiye Babuu wakitaa, na ndiye handsome wetu kwa wiki ile iyopita, Babuu alikuwa anashindana na Adamu Mchomvu na alimzidi kwa kupata kura 30(57%) na Adamu yeye kupata kura 22(42%.) Asanteni kwa wadau wote wa Blog hii kwa kuvote.

QUEEN OF DANCEHALL NIGHT

Jumamosi hii pale Zhong Hua Garden patakuwa hapatoshi kwani atatafutwa kimwana anayejua kucheza mziki wa Dancehall, so don't miss hiki kitu cha kuukaribisha mwezi wa 12.

KILA JUMAPILI USIKOSE KUITEMBELEA BAND YAKO YA TOPBAND.


Inter-College Special 2009 YAACHA GUMZO MAENEO YA KAWE.

D' Banj akiwa na mwenzake kutoka Nigeria walifanya show nzuri na ulipofikia wimbo wa Falling Love sidhani kama kuna mtu alikaa chini.

Belle 9 ndio msanii aliyefungua dimba la wasanii wa east africa kuingia kwenye jukwaa.

Kijana marlaw aliwakilisha vizuri kwa kuimba na kulitawala steji

Quick Rocka msanii ninayemkubali alipanda stejini akiwa na nguvu zote huku kwenye mtambo alikuwa dj choka akimfanyia show yake, usipimeeeeeeee

Nyomi hilo

B Dozen, B12, B Twangala, the KinG of afternOOn shOw akiwa kwenye jukwaa.

Braza wa Ma crank Cpwaa niliipenda show yake

Ally Kiba mzee wa Pamba, Mutu wa watu,

TID aka Top In Dar aka Top in Jail akiwa kwa steji

Joh Makini mwamba wa kaskazini alipanda kwenye steji na msanii wenzake wa Atown Gnako, na show aliyoitoa usiipimie kabisaaaaaaa

Gnako aka G gwala gwala.

Yuko Kerorooooooo, nikutoka Nairobi - Kenya anaitwa Nonini alipata shwangwe zakutosha kabisa

Kutoka Nairobi tena anaitwa Nameless akiwaambia mabinti huwa anasinzia akiwa anawawaza.

Mpango mzima ukafikia kwa Cowbama Mangwear alipopandishwa na dj choka 4 da 1 & 2, show ilikuwa kali zaidi alipopanda mtoto wa kitaa BAbuU.

Piga Nduruuuuuuuuuuuuuuu, ikafikia zamu ya Jua Kali kutoka Nairobi - Kenya, show ilikuwa poa sana na nduru zilisikika kila kona, BIG UP BRO.

SHAVU LA Inter-College bUSH.

dj choka na romeo jons

Odile na Producer Luchi

Steve Kafaya(East Radio) &
B12 (Clouds FM), hawa ndio waliokuwa ma MC wetu kwa siko hiyo.

Belle 9 na Mangwear

Nisikilize mimi wewe dogo, huo ndio mkwara aliokuwa anapigwa nao Romeo na Babuu wakitaa.

Unabishaaaaaaa.

Neema, dj choka & Annie

TID, CPwaa & Mangwear

Nonini, djchoka & Nameless

Romeo, Mangwear, Quick Rocka na B12

Top Band

Babuu wa kitaa, Ngwear, Ludewa na Nas 3

THT Dances

MCHANA HUU D BANJ ALITEMBELEA VIWANJA VYA TTC

Friday, November 27, 2009

Huu ni mkutano uliofanyika mchana huu na kuzungumzia show nzima kwa jinsi itakavyokuwa kesho pale Tanganyika Packers Ground (Kawe). Tamasha hili ambalo limepewa jina la STR8MUZIK - Inter-College Special 2009 litakuwa na wasanii kibao wakiongozwa na D Banj (Nigeria), Nonini, Juacali and Nameless (Kenya), Mangwea, T.I.D, Quick Racker, Belle 9, Marlaw, Cpwaa,Joh Makini , THT, BEST FRIENDand 2 Suprise artist

Nonini akifuatilia habari kwa ukamilifu.

D Banj alikuwa ananiuliza kuhusu chakula gani ale ashibe coz mimi najiita Mr. Apetite.

Jukwaa lenyewe ndio hili likiwa kwenye hatua za mwisho.

HABARI ZILIZONIFIKIA HIVI PUNDE ZINASEMA
TIKETI NI SH 3500/= NA UTAPATA BIA 3 MLANGONI...hii ni Eid Adhuhuna
Ilaleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.

SHOW ME WHAT YOU GOT SON.

INGAWA AMEZALIWA LEO..

Jay Moe msanii mwenye kipaji pekee akiwa amezaliwa leo jamaa nilimtafuta na akaniambia hayupo Dar yupo porini huko akiwa na wasanii wenzake Ferooz na Afande Selle. Jay Moe ameniambia leo wanapiga KARAGWE, kesho kwenye sikukuu ya Eid wanapiga BUKOBA mjini halafu mchakamchaka unaendelea NGARA, CHATO, GEITA, SHINYANGA na NZEGA.

BUSTA RHYMES HAKUREMBA ALIPOINGIA KWENYE JUKWAA LA FIESTA ONE LOVE 09.




PART 2.


TANZANIA & KENYA INDEPENDENCE DAY.

KWA WALE WOTE WAPENDA RAGGA & REGGAE.

Thursday, November 26, 2009

Kituo kipya cha maraha kimefunguliwa na hii ni kwa wote waliokuwa wanamiss kuruka kwanja za Ragga & Regga, hii itakuwa kila Ijumaa maeneo ya Hunters Club.

VICHWA VIWILI VINAKUTANA KESHO.

Njoo utizame show kali yenye kuunganisha vichwa viwili namzungumzia Fid Q na Mzungu Kichaa, mahali ni pale Russian-Tanzania Cultural Center (Ocean View) kuanzia saa tatu usiku

WIMBO MPYA WA NAKO 2 NAKO.

From A-City To Dar City…. Lord, Gnako and BuNako are hot regardless of location. In two years time they have gon thru major deterioration from group disintegration to internal conflicts. But cleaning up their act with good music is what hip hop is all about. This is their second release this year and its from B’Hits music. The first release was more educational but this one is all about having a good time….NDANI YA NYUMBA

ZIARA YA FID Q MJINI BAGAMOYO (KAOLE).

Huu mti unaitwa Mbuyu una miaka mingi sana tena umeshavuka karne.

Aliyekaa katikati ni Makamua msanii wa bongo fleva ambaye kwa sasa yuko Bagamoyo anakula kitabu kidogo, tulimkuta huku na tukamuomba tuwe nae katika kujifunza mambo mawili matatu, hapa tulikuwa tunapewa somo kabla yakuanza kutembea.

Shabiki wa Fid Q akiwa na bwana farid

Kama unavyojionea makaburi ya viongozi wa zamani, hapa tuliambiwa kaburi lenye mnara mrefu kuliko wenzake basi huyo alikuwa kiongozi mkubwa sana kwa wakati huo.

Michael wa Babkubwa akiwa na Edmond Azaza, hawa nao tulikuwa nao katika safari yetu.

Hapa alipokaa dj choka ni Kaburi la mke na mume (Wapendanao), kaburi hili wamezikwa mume na mke waliokufa siku moja kwa ajali katika bahari ya Hindi na kuzikwa kwa Pamoja.

Fid Q akiwa kwenye pozi la kihistoria nyuma yake ndio hayo makaburi ya watu wazamani.

Hapa washkaji walikuwa kwenye kisima ambacho hakijawahi kukauka maji na wanasema maji hayo huwa yapo hivyo hivyo hata huyapunguze vipi, washkaji wakinawa kwa pamoja.

Fid Q akichota na yeye hayo maji na kuanza kunawa, picha hii walikuwa wakinawa na Michael aka M X

Timu nzima iliyomsindikiza Fid Q ikiwa kwenye pozi la pamoja.

Baadae tuliingia kwenye gereza ambalo mababu zetu walikuwa humo, hapa fid akiwa anaionyesha picha ya ABUSHIRI, huyu alikuwa mfanyabiashara mashuhuri katika eneo la mwambao mwa afrika ya mashariki kuanzia Bagamoyo hadi Tanga.

Hapa ni nje ya gereza hilo kama unavyojionea sanamu la mfungwa akiwa amebeba pembe ya ndovu.

Unabishaaaaaaaaaaaa... baada ya kuzunguka kote tukapitia msosi kidogo, mimi hapa ndio nashiba. Kaa humo

MAHALI PA KUJIRUSHA SIKU YA EID EL HAJJ.

BANGI MARUFUKU KUVUTWA BONGO REC.

P. Funk Majani amepiga marufuku uvutaji wa bangi kwenye studio yake ya Bongo Rec, jana majira ya jioni nilimtembelea na kukuta karatasi iliyobandikwa kwenye mlango wakuingia studio.
Hapa alikuwa anaonyesha msisitizo wa nguvu na ole wako ubisheeeeee

Kama unavyoliona hilo karatasi hapo pembeni kulia.

SHOW ILIYOFANYIKA KATIKA CHUO CHA SANAA BAGAMOYO (TASUBA - Taasisi ya Sanaa na Utamaduni)

Mashabiki wakiwa jukwaani na mwanadada Ray C

Ray C

Fid Q ndio msanii aliyefunga show kwa siku hiyo.

Lord Eyez & dj choka

Michael na dj choka.

NANI UNAMUONA YUKO HANDSOME KATI YA HAWA HAPA KWA WIKI HII.

Wednesday, November 25, 2009

Adam Mchomvu ni mtangazaji kutoka katika radio ya Clouds FM na Babuu wakitaa yeye ni msanii wa bongo fleva napia anafanya kazi pale Clouds TV.

UNAWEZA KUVOTE KWA MTU ANAYEMPENDA HALAFU WIKI IJAYO TUTAMTAJA MSHINDI.

DJ CHOKA PRESENT BEAUTY OF THE WEEK.

Huyu ndio Beauty wa wiki iliyopita anaitwa Angeris ambaye alikuwa anashindana na mwenzake Gitta. Kura zenu zinasema hivi Angeris alipata kura 45 (63%) huku mwenzake Gitta alikuwa na kura 26 (36%) so mshindi ni ANGERIS big up dada yangu utunze huo u beauty wako.

SHUKRANI KWA WADAU WANGU MLIOKUWA MNAVOTE.

TRUE LOVE.



Jux - Nimedata (NEW VIDEO)


B'HITS YATOA RATIBA ILIYOJITOSHELEZA.

Watch Out For B'Hits New Releases..
28th Nov Nako 2 Nako-"Ndani Ya Nyumba".5th Dec Long awaited AY's-"Bed n Brekfast",also Klynn come back-"Not A flirt". 19th Dec Nick Wa Pili-"Higher" and Joh Makini's-"Show Ya Joh"...

Diamond - Kamwambie (NEW VIDEO)



VIDEO MPYA KUTOKA KWA HUSSEIN MACHOZI "UTAIPENDA"



CPwaa's PRE - LAUNCHING PARTY.

Its my pleasure to inform all BongoFlava, CPWAA's fans and local muisc supporters that i will have an exclusive pre-launching party on 8th Dec 2009 at Movenpic.

Shughuli nzima itaanza na wageni waalikwa (V.I.P) kuanzia saa 2 usiku mpaka 5 usiku na baadae kwa kiingilio cha 15,000 TSH kwa yeyote atayependa kuingia. Usiku huo kutakuwa na uzinduzi wa tovuti zangu 2, mavazi,documentary fupi, nyimbo mpya na video zake bila kusahau Album Preview na perfomance moja ya ukweliiiiii!
--
Na baada ya hapo, ngoma zote za ukweli zitapigwa na maDJ wakali kutoka jijini Dar, na shangwe hilo litaendelea mpaka kuchwele. looking forward to see you there.

Support local talents, support our music! na tutafika tu.

Cpwaa and Splif star of Flipmode squad having a good conversation at the Busta Rhymes after party, Level 8 Kempinski hotel.

TIZAMA GANGSTAR YA LANGA.


NEW VIDEO KUTOKA KWA DE PLAIZIR.



After the Hit single Swali, The King of Pleasure, drops Kende kaka meaning "Just Go" from his native Lingala language, the second single from his forthcoming album... The song features the Kora awards winning Tanzanian Deva Lady JayDee and a good mix of Congolese rumba and Salsa interpreted in swahili and lingala..

BUSTA RHYMES AMZIMIA WITNESZ.

Tuesday, November 24, 2009

Nikiwaga kule New York huwa napenda sana kumpitia huyu mshkaji wangu Spliff Star, asubuhi aliniita kunipa zawadi yangu.

Brother Joseph akiwa na mwanadada Witnesz

Witnesz na Spliff Star

DJ wa Busta & Witnesz

Madj wakali wakiwa kwenye pozi, huyu jamaa cut zake kwenye turntable hazipishani sana na mimi so nilimzimia sana.

Hapa Busta alikuwa anapewa zawadi na Brother Joseph, kama unavyoziona hapo juu.

Busta akipiga sign kwenye Biblia ya Witnesz,

Ndani ya gari ni Spliff Star akifanyiwa mahojiano na Clouds TV

KARIBUNI TENA NDUGU ZETU.

SHOW YA BUSTA NILIIPENDA SANA

Hapa alikuwa chini akijiandaa kuitwa kwa steji.

Kama unavyojionea mwenyewe.

Hapa Busta aligawa mic kwa mtanzania na kumsikiliza anachoongea.

Usiwapimie hawa jamaa daaah, nilikuwa natamani show isiishe hivi kwa makamuzi ya hawa jamaa, network kama inazingua ila nawaahidi kuweka vipande vya show yake soon.

ONE LOVE ILIVYOTIKISA JIJI.

Mr. Blue akiwa jukwaani akikamua

Hussen Machozi hakuwa nyuma, nae alihakikisha amefanya vizuri na watu walimkubali.

HBC Kazini, watu wazima wanaoheshimika hapa kwetu bongo.

Jose Mtambo akafikia zamu yake, hapa akiwa na Chidi Beenz

Chege Chigunda mtoto wa mama Said akiwa kwenye jukwaa la fiesta, Chege aliimba Live siku hiyo.

Ally Kiba nae kama kawa mfuniko wake unatakiwa umuone mwenyeweeeeee.

Marlaw nilipenda show yake sana, alijituma stejini kwa kuimba na kucheza.

Swich zote zilikuwa ON walipoingia watangazaji wa Clouds FM dj Fet na B12 na kutambulisha wasanii watakaofuata, walipendeza kinyamaaaaaaaaaaaaaaa

CP aingiapo stejini huwa harembi, hapa akiwa na vijana wa THT.

Mwanadada Shaa alifanya show kali na nzuri, kila mara alikuwa anajituma kwa kucheza na kukizungusha kiuno.

Black Rhino alipendeza kimavazi na kwenye show alifanya poa sana, BIG UP

Quick Rocka usimpimie, NO COMMENTS

Adamu MChomvu mtangazaji wa Clouds FM alipata shangwe nyingi alipoingia kwenye jukwaa

Gnako akiwa stejini, hapa alipanda yeye kwenye wimbo wa DOgo Hamidu unaoitwa 26 Number na baadae akabaki stejini akikamua mwenyewe.

Unapenda nini ili na mimi nifurahi....Jafarah akiwa stejini na mwanadada Fatma.

Wateule wakarudi tena.

Ikafika zamu ya Langa kuwa kwa steji.

King Kong kutoka Ilalaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

SHOW LOVE YA FIESTA DAR ES SALAAM.

kApiteniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii Gadna G. Habash

Hapa hata aje nani watakaa tu, mnabishaaaaaaa

Mwanadada Zamaradi alitoka poa sana.

Black Rhino akionyesha CD iliyopigwa sign na Spliff Star

Dad akiwa na Man dojo

Quick Rocka na Izzo Biznes

Rukia akiwa na shosti wake Shaa.

Quick na Suma Lee

Maproducer wawili wanaosumbua bongo kwa sasa, kushoto ni Lamar akiwa na Luchi

Luchi akiwa na braza jina limenitoka msaada kwenye tuta.

Mangwear akiwa braza Big Willy

Fanani na Mangwear

Prof Jay na Baby Madaha, watu wengine wakiwa kwenye mapozi mazuri wengine wanaandika eti hawa niwapenzi, watu bwana daah.

Langa na Babuu wakitaa.

Yang D akiwa na Cyrill

Vijana wadogo kwenye game la bongo fleva wakikutana basi huwa ni furaha tupu, Yang D na Baby Boy

Jux & Cyrill

Haya sasa ndugu yangu tuingie kazini...

B12 na Mangwear

Shemeji na Black Rhino.

Marlaw, Lamar na CP

Big Willy, Shemeji na dj choka

Vijana wakijadili jambo

Enzi zileeeeeeeeeeeeee, hapa Fanani, Bigg Willy pembeni Niggar Jay, aaaaah watu hawakai

Hatimaye One Love imewakutanisha watu wengi mfano wao ni kama hawa Daz Nundaz.

BABY POWDER MOVIE PREMIERE (Atlanta,GA)

Baby Powder, a new film produced by US-based Tanzanian film production company, Jake Productions launched in November 14 in Atlanta, USA. The cast of the movie features East Africans living in the USA mainly Tanzanians and Kenyans( also Americans,Hitians and more)

The film is about a young African man (Phillip Nkasa) who moves to the states in the hope of educating himself to improve his life and his family back home. But things don't go according to plan and he ends up getting involved in illegal business and the darker side of life .
The Cast: Lambert Tibaigana PHILIP NKASA, Tuni Ngigi WARIDI, Carlos Mwaibula TIZO, Ulimboka Mwanjabala CHUMA, Hadji Saidi WESI, Lydia Mbuah JOSELYNE, Warda Hassan JACKEY, Dynamic DULAH, Albert Levasser MAMADO, Babu Sikare KAI and many others.

HOUSTON,TX November 26th 2009
THE NEW FUNPLEX
13700 Beechnut,
Houston,TX 77083

WASHINGTON,DC December 5th 2009
TBA

WICHITA,KS December 12th 2009
WARREN THEATER

MINNESOTA,MN December 19th 2009



D BANJ LIVE IN DAR "STR8MUZIK FESTIVAL"

Performing artists, D Banj (Nigeria), Nonini, Juacali and Nameless (Kenya), Mangwea, T.I.D, Quick Rocka, Belle 9, Marlaw, Cpwaa, Joh Makini , THT, BEST FRIEND and 2 suprise artist
Transportation : Free from colleges / Universities main campuses

Location : Tanganyika Packers Ground(Kawe)
Date : Saturday, November 28, 2009
Time : at 5:00pm
Entrance’s 3500/=

MACHOZI BAND NEW VIDEO "MTALIMBO"



JOH MAKINI "STIMU ZIMELIPIWA"



ONYO NA TAHADHARI KWA WASHKAJI ZANGU WA FACEBOOK

Friday, November 20, 2009

Kwenye Facebook kuna mtu analitumia jina langu na kujifanya kwamba yeye ndiye Mr. Blue, napenda kuwataharifu kwamba ukiliona jina limeandikwa MRBLU CABYCER ujue sio mimi huyo, mimi natumia jina la HERRY SAMEER, na utaiona picha kama hii iliyopo hapa kwenye blog ya dj choka. Huyo mtu hata simjui na sijui kwanini kaamua kulitumia jina hilo la kwangu.

HBC SINCE 1990.

Tshet mpya za Prof Jay zilizo na maandishi ya HBC SINCE 1990 sasa zimekamilika na zipo tayari, soon nitawaambia zinapopatikana kwa wanaozitaka.

Prof Jay akiwa na mshkaji wake leo asubuhi.