22.11.13

Saturday, July 10, 2010

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


ZIFF KUANZA LEO (TAREHE 10 July 2010)

“KIINGILIO BURE”

Tamasha la 13 la filamu limepangwa kuanza leo tarehe 10 Julai 2010 katika uwanja wa Ngome Kongwe ulioko mji mkongwe mjini Zanzibar.

Tamasha hili lenye msisimko linatazamiwa kuhudhuriwa na zaidi ya wageni 200,000 likishirikisha zaidi ya nchi 43, hivyo kuwa tamasha kubwa lenye msisimko wa aina yake.

WAGENI WATAKO UPAMBA UFUNGUZI WA TAMASHA HILI NI:
STEVEN KANUMBA
EVONNY CHERRY YAKUB (MONA LISA)
VICENT KIGOSI


Zaidi ya Filamu100 zitakazoonyeshwa mwaka huu katika tamasha linalotazamiwa kukoma tarehe 18 July 2010.

Filamu ya ufunguzi
Filamu itakayo fungua pazia la tamasha hilo Mwaka huu ni

Youssou N’Dour: I Bring What I Love
Iliyoongozwa na: Elizabeth Chai Vasarhelyi
Filamu itaonyeshwa 10th July, Old Fort, Kuanzia saa 3:00 usiku baada ya ufunguzi rasmi.


Filamu hiyo ya ufunguzi, ni filamu yenye tunzo nyingi. Filamu hiyo inayo muhusu mwanamziki maarufu Youssou N’Dour, I Bring What I love (Naleta nachokipenda), inayozungumzia imani na amani. (addresses the themes of religious tolerance, harmony and peace.) ina lengo la kuhamasisha, inaonysha safari ya kimziki, yenye ushuhuda wa nguvu ya sauti ya mtu mmoja kuhamasisha mamilioni.

“I Bring What I Love” imedhaminiwa na SIGNIS.

FILAMU NYINGINE KUBWA ZITAKAZO ONYESHWA MWAKA HUU NI:

Nipe Jibu: Kuonyeshwa kwa mara ya kwanza . Filamu ya kwanza ya kuchanganya Muziki na kuigiza Muongozaji Nadine Louise Fasera. Nipe Jibu ni filamu nzuri ya Kiswahili yenye kuchanganya muziki iliyotengenezwa kwa mtazamo wa kisasa na kitamaduni kwa simulizi iliyochangamka juu ya binti yatima anayeishi kwenye maisha ya ndoto.

My Policy: Kuonyeshwa kwa mara ya kwanza. Kijana mdogo mfanya biashara anapigwa risasi kwenye siku yake ya kuzaliwa akiwa anarejea nyumbani kwake akitokea kwenye tafrija yake kusherehekea siku hii muhimu akiwa na mchumba wake, Victoria. Wiki chache baadae, Yule aliyempiga risasi amjia na kumchoma kisu hadi kufa. Kwa kupagawa na pigo hili, Victoria aamua kuhama Montreal na kuanza maisha mapya, Lakini muuaji amjia nay eye pia.... Muongozaji: Phad Mutumba

Motherland: African premiere - Kuonyeshwa kwa mara ya kwanza Afrika

Ana’s Playground: - kuonyeshwa kwa mara ya kwanza Afrika

Lamu’s Maulid: Kuonyeshwa kwa mara ya kwanza kidunia: world premiere

Inside Life: : Kuonyeshwa kwa mara ya kwanza kidunia: world premiere
Pumzi: East Africa’s first ever science fiction film
A sneak preview of Twiga Stars

Vitu Vya Kutazamia Mwaka Huu:
Kutokana na kufahamu umuhimu wa mashindano ya Mpira Kombe la dunia
Tamasha la ZIFF 2010 litaonyesha Fainali ya Kombe la dunia! KWENYE SCREEN KUBWA.
Fainali hizo zitashuhudiwa katika uwanja wa wazi wa kome kongwe kwenye uzinduzi wa tamasha hili la mwaka huu 2010. Kwa wapenzi wa soka kazi kwenu
KAULI MBIU YA ZIFF MWAKA HUU: ina angaza matakwa ya watu wa kisiwa cha Zanzibar ya amani na muafaka kufuatia kipindi cha uchaguzi.

Muziki
ZIFF 2010 Itakua ikisakata kwenye burudani ya muziki na Dully Sykes – AKA Mr Misifa ama Mr Chicks, Msanii anayetambulika sana kwa miondoko ya dancehall Tanzania. AY, Msanii anayengara ndani ya Africa Mashariki akiwakilisha vyema Tanznia na balozi wa burudani Tanzania, Kidumu , Ndiye mwanamuziki maarufu Africa Mashariki toka Burundi anayeshikilia Tunzo nyingi ikiwemo tunzo ya Muziki bora wa Afrika Mashariki kwa Tunzo za Tanzania Music Awards, Body Mind Soul Bendi ya watu 6 kutoka Kaskazini mwa Malawi wanaopiga mziki wa kiafrika wenye vionjo vya Jazz, Windhund featuring Sekembuke & Siga bendi kutoka Austria inayotumia vionjo vya kizungu na kiafrika, ushairi na sanaa ya simulizi ili kuleto vionjo vipya na vya aina yake kwenye ulimwengu wa muziki.

Filamu za Watoto!
Kwa kushirikiana na taasisi ya filamu ya Kidanish, Maonyesho ya filamu za Watoto zitaonyeshwa makundi makubwa ya Watoto, zikiwa zimetafsiriwa kwa Kiswahili kwajili ya Watoto na vijana wa Mji mkongwe.

Art exhibtions
"Hopes in Harmony" (Matumaini yenye Kuafikiana) – Onyesho la picha yanayoletwa na mpiga picha toka Italy, Carlo Deste"Colour Bash" – Uchoraji wa vitenge kutoka pande mbalimbali za Afrika, na Mahelia de Randamie Artwork kutoka wakina mama wa Iranian, Hii inaletwa na Ubalozi wa Iranian embassykwa kushirikiana na Soko Filam, ambapo watengeneza filamu na wachongaji toka Zanzibar wanakuja kuonyesha na kuuza bidhaa zao..

Tasnia
ZIFF ni tukio muimu kwenye jumuiya ya Cinema duniani. Festival Forum na Festival of Festival program inatoa nafasi kwa wasambazaji, mapromota, waongozaji wa filamu na waandaji kukutana ili kukomaza mizizi kwenye tasnia ya filamu kwenye nchi zinazoendelea. Mwaka huu wawakilishi toka Trinidad na Tobago, Uganda, Holland, Iran, Mexico and Italy watashiriki ZIFF kujadili nafasi ya matamasha ya filamu kwenye nchi zinazoendelea.

Warsha
ZIFF itaendesha warsha tatu wakitoa upendeleo kwa ushiriki wa waandaji filamu toka ukanda huu wa Afrika mashariki kwa waandaji wenye kuonyesha hari na vipaji vyenye mlengo wa kuibuka kwenye tasnia hii.

WARSHA ZA NAMNA YA KUOMBA MISAADA YA KIFEDHA KUANDAA FILAMU NA WARSHA – warsha itaongozwa na wakufunzi toka Sweden and Uganda

UANDAAJI WA MAKALA: CONNIE FIELD – Warsha hii ya siku nzima italeta mtazamo mzima wa namna ya kuandaa makala chini ya usimamizi wa mshikiliaji wa tunzo ya uandaaji wa makala(producer / director), Connie Field.

CINEPHILMS:UTENGENEZAJI WA FILAMU KUTUMIA SIMU YA MKONONI – Hii warsha ya aina yake itaongozwa na Jonathan Dockney wa chuo kikuu cha Natal South Africa. Utengenezaji wa filamu kwa kutumia simu za mkononi ni teknolojia inayo ibuka kwa kasi sana. Njo ujifunze jinsi ya kutengeneza filamu kwa simu!

Tafadhali bonyeza hapa kwa maelezo zaidi: http://www.ziff.or.tz/ ama www.ziff.or.tz/press

KWA ZIADA WASILIANA NA:
Asmah Makau
Afisa Habari (Swahili Press)
asmahmakau@yahoo.co.in Tel no: 0713711413 / 0767711413
Laura Martin-Robinson (English language Press)
press@ziff.or.tz
Tel: +255 782689845


RATIBA YA SIKU YA UFUNGUZI

TIME

WHO/ WHAT
7:00-8:00
Background music, Trailers

ZIFF team
8:00-8:02
Opening presentation

MC Hassan and Linda
8:02-8:07
Video ZIFF Biography

ZIFF technical team
8:07-8:08
MC presentation music act

MCs
8:08-8:13
MUSIC

KJETIL HAUGBRO
8:14-
MC presenting Chairperson

MCs
8:15-8:18
Speech by the Chairperson

Mr Mitawi
8:18-
CHAIRPERSON presenting CEO

Martin Mhando
8:18-8:21
Mr. Mhando launches ZIFF 2010

DHOW sail and fires
8:25-
MC presentation Zanzibar Poetry

MCs
8:26-8:31
ZANZIBAR POETRY

Amina
8:32
MC presenting GUEST of HONOR

MCs
8:32-8:37
Guest of HONOR SPEECH


8:37-
MC presenting dance act

MCs
8:38-8:45
DANCE group Zanzibar

D six group
8:45-
MC calls SIGNIS representative on stage

MCs
8:46-8:51
SIGNIS present the opening film

SIGNIS JURY
8:51-10:20
Launch of the opening film
Greetings by MCs Happy Tamash
a !!!

No comments: